MSIKIE RONALDINHO KUHUSU MESSI NA RONALDO . NA NINI ALIKIKOSA ENZI ZAKE

Katika mahojiano ambayo nyota wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Ronaldinho Gaucho ameyafanya na jarida la SPORTS la Hispania ameongelea mambo mengi kuhusu soka la sasa.
Kati ya mambo ambayo Dinho amesema ni kwanza mchezaji ambaye anatamani angecheza naye katika kipindi chake ila hakucheza naye. Dinho amemtaja kiungo wa klabu ya Barcelona Phellipe Coutinho kama kiungo ambaye angefanya mchezo wa soka kuwa rahisi kwake kama wangecheza pamoja. Fundi huyo wa soka anaamini Iniesta na Coutinho ni kati ya viungo bora sana ambao amewahi kuwaona katika soka na Coutinho atakuja kuwa moja katika ya wachezaji wakubwa sana duniani siku za karibuni. Lakini mtangazaji aliamua kumuuliza Ronaldinho swali ambalo pengine kila mtu wa soka amewahi kuulizwa ama kuuliza, hivi Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ni yupi unamkubali?
“Kwangu mimi sipendi sana swali hili lakini ukiwaangalia hawa watu wawili nadhani mimi navutiwa zaidi na namna Lionel Messi anavyocheza “. Ronaldinho amesema kuhusu Cristiano Ronaldo ni mchezaji ambaye amekamilika na ana kila kitu uwanjani kama ilivyo Messi ila bado yeye anamuona Messi anavutia zaidi kumuangalia.
Lionel Messi hapo jana aliongoza mauaji ya Barcelona walipoipiga Huesca bao 8-2 na sasa Muargentina anakuwa nyota wa kwanza kufikisha assists 150 La Liga.

Post a Comment

0 Comments