‘Gari iliyomteka MO imetambuliwa, mmiliki na dereva wanafahamika’ IGP Sirro

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema jeshi hilo limefanikiwa kutambua aina ya gari ambalo limetajwa kumteka mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji pamoja na dereva aliyekuwa akiendesha gari hiyo aina ya Surf. IGP Sirro amesema jeshi hilo kupitia vyombo vya uchunguzi vilifanikiwa kukamata ganda la risasi yenye urefu wa Milimita 9 ambazo zilitumika wakati wa tukio la kupotea kwa Mohamed Dewji. Kamanda Sirro amesema gari hilo limesajiliwa kwa namba za usajili za kutoka nchi jirani ambapo inaelezwa gari hilo lilifanikiwa kuingia mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu. “CCTV camera zimetusaidia zimeweza kutambua gari baada ya kufanya uchunguzi tumefanikiwa kulijua gari na tumezungukia maeneo yote ambayo hilo gari lilipita na bado watu wetu wameendelea kufatilia kama gari lilielekea maeneo ya Silver sand au Kawe.” “Ila tumepata taarifa kwamba gari hilo limetokea nchi jirani, na watu wetu wamekwenda mpakani na wameona gari hii likipita mpakani tarehe moja septemba. Nani alikuwa dereva wa ile gari imefahamika”

Post a Comment

0 Comments