we bring music and news for life


 

TRENDING

2018/12/09

ALIKIBA ANG'ARA COASTAL UNION IKIKIPIGA DHIDI YA MBEYA CITY FC


Staa wa Bongofleva Alikiba leo Jumapili ya December 9 2018 ilikuwa siku ya kwanza kuichezea Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara, mchezo ambao ulichezwa katika uwanja wa Mkwakwani Tanga dhidi ya Mbeya City, baada ya kufanya mazoezi pamoja na wenzake kwa wiki moja. Alikiba akiichezea Coastal Union ndani ya dakika 5 za kwanza akasababisha kona iliyokwenda kupigwa na Athumani Iddi Chuji na kufungwa kwa kichwa na Ayoub Lyanga, goli hilo la Coastal Union lilidumu kwa dakika 50 ambapo Mbeya City walisawazisha kwa Bakari Mwamnyeto wa Coastal Union kujifunga. Game hiyo iliyomalizika kwa sare ya 1-1, Alikiba alicheza kwa dakika 64 na kocha Juma Mgunda akafanya mabadiliko ya kumtoa Alikiba na kumuingiza Deo Anthony, hii ndio mara ya kwanza kwa Alikiba kucheza kwa dakika zaidi ya 60 mechi ya Ligi Kuu hivyo ametimiza ndoto yake ya muda mrefu kucheza soka la ushindani, Alikiba pia ni mdhamini wa Coastal Union kupitia kinywaji chake cha Mofaya. 

No comments:

Post a Comment

Pages