Dembele ndio mchezaji anayeongoza kwa kupigwa faini Barcelona

Winga wa FC Barcelona Ousmane Dembele anatajwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji wachache wanaoshindwa kuishi maisha ya kuwa professional katika kazi yao ya soka, Dembele imeripotiwa kuwa ndio mchezaji wa Barcelona ambaye anaongoza kwa kupigwa faini. Dembele ambaye ana umri wa miaka 21 aliwasili FC Barcelona miezi 18 iliyopita akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani lakini amekuwa ndio mchezaji ambaye anatatizo la kutotunza muda na kufika mazoezini na sehemu mbalimbali za majukumu yake nje ya muda.
Ndani ya miezi 18 aliyokuwepo ndani ya Nou Camp, Ousmane Dembele anadaiwa kupigwa faini inayodaiwa kufikia jumla ya euro 50000 ambazo ni zaidi ya Tsh Milioni 130, Dembele Jumapili iliyopita alichelewa kwa saa mbili mazoezi ya kuelekea mchezo dhidi ya Espanyol na mwezi October ndio aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa Barcelona aliyepigwa faini zaidi.

Post a Comment

0 Comments