MOTO WA MESSI HAKUNAGA ULAYA


Umri wake unakwenda, kasi yake bado inadai. Huyu jamaa uwezo wake utadhani amekata breki. Anatisha sana huyu kiumbe. Alipoondoka Ronaldo kule La liga wengi walidhani Lapurga atapunguza kasi. La hasha! msimu huu Messi anaongoza kwa kufunga magoli mengi ya mpira wa adhabu ligi zote kubwa barani Ulaya 🇦🇷 Lionel Messi (3) 🇷🇸 Aleksandar Kolarov (2) 🇨🇭 Granit Xhaka (2) 🇳🇱 Memphis Depay (2) 🇸🇰 Ondrej Duda (2) Kwa kuongezea tu: Mwaka 2018 amefunga magoli 10 ya faulo idadi kubwa zaidi katika kalenda ya mwaka kwenye maisha yake ya soka. Msimu huu amekwisha husika katika magolo 27 kwenye michezo 17 tu, hatari sana huyu mwanadamu.

Mwisho sasa: Messi amekuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya la liga kufunga zaidi ya magoli 10 kila msimu kwa miaka 13 mfululizo. Pata kifurushi: Takwimu za Messi Barcelona ✍️Mechi: 654 ⚽Magoli: 569 🎯Assists: 226

Post a Comment

0 Comments