MSIWASUMBUE WAMACHINGA,MAMA LISHE " RAIS MAGUFULI "

Rais Dkt. John Magufuli ametoa vitambulisho maalum kwa ajili ya kuwatambua wafanyabiashara wadogo wadogo nchini ambapo kila Mkuu wa Mkoa atakabidhiwa vitambulisho Elfu 25 na kila kitambulisho kitagharimu shilingi elfu ishirini. “Kuanzia leo Wafanyabiashara wadogo watakuwa na vitambulisho sioni Wafanyabiashara wadogo wakisumbuliwa na mtu yoyote vipo vitambulisho 670000 kila Mkuu wa Mkoa ataondoka na Vitambulisho elfu 25,000” Rais Magufuli “Agizo langu la kusajili wafanyabiashara wadogo wadogo linakwenda taratibu sana. Sasa naona suala la vitambulisho vyao mmevichanganya na vitambulisho vya taifa, mmefanya hivi ili tu mcheleweshe. Naomba wafanyabiashara wadogo wasisumbuliwe” Rais Magufuli ”Unakuta Mamalishe ana mtaji mdogo au machinga anauza pipi lakini kila siku wanafuatwa kulipa kodi, nimesema wapewe vitambulisho lakini mnachelewesha sana” Rais Magufuli “Nimezungumza mno hao wafanyabiashara wadogo wadogo msiwasumbue ukiacha wale wanaobeba bidhaa za Wafanyabiashara wakubwa. Ila huwezi kuwasumbua Mama Lishe, Wauza mchicha na mihogo” Rais Magufuli

Post a Comment

0 Comments