Mtoto hatumwi dukani: Liverpool vs Napoli

Leo jumanne, Ligi ya Mabingwa barani Ulaya itaendelea tena. Kutakuwa na mechi nane usiku wa leo. Moja ya mechi inayosubiriwa na watu wengi, ni ile ya kundi la kifo( kundi C) ambalo Liverpool wanawakaribisha Napoli.
Napoli hawajawahi kushinda England kwenye mechi zao sits walizocheza. Wanaongoza kundi C wakiwa na pointi tisa, wakifuatiwa na PSG ambaye ana pointi nane, Liverpool wana pointi sita, wakati Red Star Belgrade wana pointi nne. Liverpool ili wafuzu hatua ya 16 bora, wanahitaji kumfunga Napoli 1-0 au 2-0. Maana yake wasiruhusu goli lolote. Wakati Napoli wao wanahitaji sare tu.
Tukumbuke Liverpool wamefungwa mechi tatu za Ugenini kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu. Kipigo cha 1-0 dhidi ya Napoli, wamefungwa na Red Star goli 2-0, halafu wwkafungwa 2-1 na PSG. Najua Liverpool kupindua matokeo sio kazi kubwa kwao hasa ukizingatia wako uwanjani kwao Anfield. Pia wataomba PSG atoe sare dhidi ya Red Star. Red Star hata akishinda haendi popote. Hivyo watakaoamua matokeo ya kundi C ni Liverpool na Napoli.
Liverpool kulinda goli lao lisiguswe inawezekana ila inategemea watacheza na Napoli ya aina gani. Napoli ni wazuri sana kwenye mashambulizi ya kushitukiza na wako imara kwenye kuzuia pia. Tisitegemee mchezo wa kupaki basi maana timu zote zitahitaji kushambulia na kujilinda kwa pamoja. Kocha wa Napoli Carlo Ancelotti hajafungwa kwenye mechi 12 zilizopita na ni miongoni mwa makocha watatu walioshinda Kombe la Ligi ya Mabingwa mara tatu. Ancelotti ameshinda akiwa Ac Milan mara mbili na mara moja akiwa na Real Madrid.
Wachezajia wa Liverpool na ambao wamewahi kucheza pamoja kwenye Ligi Kuu Italia ni Alson Barker( Roma 2016- 2018) Xherdan Shaqiri ( Inter Milan 2015 Wachezaji ambao wamecheza pamoja kwenye Ligi Kuu England ni Vlad Chiriches( Tottenham 2013-2015 na David Ospina 2014-2018)
Wachezaji ambao wamecheza kwenye Klabu moja ni Sadio Mane na Kalidou Koulibaly( Metz 2011/2012, Georginio Wijnaldum na Dries Mertens( PSV Eindhoven 2011/2013) Fabinho, Jose Callejon, Raul Albiol ( Real Madrid 2012/2013) Wachezaji ambao wanacheza timu moja ya Taifa Divock Origi, Simon Mignolet, Dries Martens( Ubelgiji) Sadio Mane na Koulibaly( Senegal) Alberto Moreno, Jose Callejo na Raul Albiol ( Hispania) Dejan Lovren na Marco Roj ( Croatia)

Post a Comment

0 Comments