Neymar kasaini dili litakalomzuia kwenda Real Madrid na Barcelona


Tukiwa tunaelekea kufunguliwa kwa dirisha la usajili la mwezi January Neymar alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuchukua headlines za kuihama Paris Saint Germain na kujiunga na Real Madrid ya Hispania, hiyo ni baada ya kuhusishwa na Real Madrid toka dirisha la usajili la majira ya joto. Kusaini kwa Neymar kwa mkataba wa matangazo ya kibiashara na National Bank Of Qatar kunaondoa nafasi ya Neymar kuihama PSG hivi karibuni, Neymar yupo PSG timu ambayo inamilikiwa na familia ya kifalme ya Qatar, hivyo mkataba wake na QNB unatajwa hauwezi kuruhusu aende nje ya PSG.
Mkataba huo ambao baadhi ya vipengele vimewekwa kama siri, vinatajwa kuipa haki Bank hiyo ya kusimamia hakimiliki ya picha za Neymar, hata hivyo uwezekano unakuwa mdogo wa Neymar kuondoka PSG kutokana na QNB kutaka staa huyo abakia PSG kwani wanaidhamini timu hivyo ni rahisi kwa wao kunufaika na ubalozi wa Neymar akiwa anaicheze timu wanayoidhamini.

Post a Comment

0 Comments