Ronaldo akana kumkumbuka Lionel Messi

Ikiwa ni miezi kadhaa imepita toka staa wa soka wa Juventus ya Italia Cristiano Ronaldo ahame Real Madrid na kujiunga na Juventus kwa mkataba wa miaka mitano, Ronaldo wakati akiwa Hispania alikuwa akitajwa kama mshindano mkuu wa Lionel Messi hiyo inatokana na wawili hao kutawala Ballon d’Or kwa miaka 10. Unaweza ukashangazwa na kauli ya Cristiano Ronaldo baada ya kuulizwa kama anammiss Lionel Messi ambaye alikuwa mshindani wake mkuu Hispania, Ronaldo alikataa na kusema kuwa labda Messi ndio amemkumbuka yeye lakini sio yeye kumkumbuka Lionel Messi, hiyo ilikuwa wakati wa mahojiano na Gazzetta Dello Sport.
“Hapana labda yeye ndio ananikumbuka, Nimecheza England, Hispania, Ureno na timu ya taifa lakini yeye amekuwa Hispania labda huenda yeye ndio akawa ananihitaji mimi zaidi, kwangu maisha ni changamoto na nazipenda na napenda watu wafurahi, ningependa kumuona akija kucheza Italia (Messi) kama mimi nilivyokubali changamoto”>>> Ronaldo Ronaldo aliondoka kwa uhamisho wa kushitukiza kutoka Real Madrid na kujiunga na Juventus msimu huu kwa ada ya uhamisho wa euro milioni 100, Ronaldo ni miongoni mwa wachezaji wa Juventus walioiongoza katika Serie A kucheza michezo 15, kushinda 14 na kutoka sare mchezo mmoja pekee wakiwa hawajapoteza game. 

Post a Comment

0 Comments