we bring music and news for life


 

TRENDING

2018/12/09

SIKU YA UHURU: Hashim Rungwe atoa tamko la vyama vya siasa “Tunapinga” (+Video)


Leo December 9, 2018 Vyama vya siasa 15 vimeungana kwa pamoja na kutoa tamko kuhusu kupinga Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ambao umesomwa Bungeni November 16, 2018. Katika tamko hilo, lililosomwa na Mwenyekiti wa chama cha CHAUMMA, Hashim Rungwe kwa niaba ya vyama hivyo ikiwemo CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI kwa pamoja wameadhimia kupinga muswada huo. “Tumeitumia siku ya leo ya uhuru kutoa tamko hili kwani ni siku muhimu kwa taifa letu pamoja na utawala wa awamu ya tano kuendelea kufuta sherehe za uhuru ambazo duniani kote nchi hutakiwa kuikumbukaa siku hii kwani ndio siku taifa linakuwa limezaliwa,”amesema Rungwe kwa niaba ya wenzake. Katika maadhimio hayo, Rungwe ametaja sababu tano za kupinga muswada huo ikiwemo muswada kukiuka Katiba ya nchi inayotoa uhuru wa kujumuika na kuunda vyama vya siasa, vyama vya siasa kutoshirikishwa katika mchakato wote wa kuandaliwa kwa muswada huo.
 

No comments:

Post a Comment

Pages