Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 23.12.2018: Ozil, Fred, Sancho, Rashford, Fekir, Pochettino


Klabu ya Uturuki ya Istanbul Basaksehir huenda ikatoa ofa kwa mchezaji wa Arsenal Mesut Ozil, 30. Rais wa kalabu hiyo alisema watafanya kila wawezalo kumpata (Bild via FourFourTwo) Ajenti wa kiungo cha kati wa Manchester United Fred anasema mchezaji huyo wa miaka 25 atasalia kwenye klabu hiyo wa Premia. Raia huyo wa Brazil alijiunga na Old Trafford mwezi Juni lakini amehusishwa na kuondoka. (Sunday Star) Mchezaji anayezozaniwa na Bournemouth na Chelsea Nahodha wa England Harry kane na Meneja Gareth Southgate wote watapewa tuzo za mwaka mpya za OBE. (Sun on Sunday) Haki miliki ya picha Getty Images
Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich wote wanammzea mate mshambuliaji wa miaka 18 raia wa England Jadon Sancho, ambaye kwa sasa yuko Borussia Dortmund. (Marca) Isco, 26, anapanga kuhamia Manchester City wakati anahofia nafasi yake huko Real Madrid ikiwa watamleta kiungo wa kati Mbelgiji Eden Hazard kutoka Chelsea. (Sunday Express) Meneja mpya wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anamfuatilia mshambuliaji wa Bournemouth John King 26, kama mchezaji anayelengwa mwezi Januari. (Sun on Sunday)
Barcelona wako tayari kutangaza ofa ya kumsainia mshambuliaji wa England Marcus Rashford huku Real Madrid nao wakimzea mate mchezaji huyo mwenye miaka 21. (Sunday Express) Mmiliki wa Fulham Shahid Khan atatangza ofa mpya ya pauni milioni 600 kuchukua umiliki wa Wembley mwaka mpya. (Sun on Sunday) Paris St-Germain wanafikiria kumsaini kiungo wa kati wa Everton Idrissa Gana Gueye. Raia huyo wa senegal mwenye miaka 29 alijiunga na Everton mwaka 2016. (Sky Sports)
Mchezaji wa Lyon Nabil Fekir, 25, analengwa na Chelsea mwezi Januari miezi kadhaa baada ya jaribio la kuhamia Liverpool kufeli. (Mail on Sunday) Kiungo wa kati wa Chelsea Dennis Wise anasea klabua hiyo itajaribu kumsaini aidha mshambualiaji wa Leicester Jamie Vardy, 31, au straika wa Bayern Munich Robert Lewandowski, 30, mwezi Januari. (Sunday Express) Meneja wa Leicester Claude Puel anasema hana lingine la kuthibitisha baada ya kikosi chake kuishinda Chelsea licha ya uvumi kuwa anajaribu kufutwa. (Mail on Sunday)
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anasema ana uhusiano mzuri na mwenyekiti Daniel Levy. Raia huyo wa Argentina anahusishwa na nafasi iliyo wazi ya umeneja huko Manchester United. (Sky Sports) Jose Mourinho anaamini alikuwa anaenda kuzungumzia sera z kununua wachezaji kwenye mkutano ambao ulinfuta kama meneja wa Manchester United. (Times - subscription required)

Post a Comment

0 Comments