TETESI ZA USAJILI LEO JUMATATU TAR.10-12-2018 BARANI ULAYA

Chelsea watamuuza Victor Moses mwezi ujao huku Crystal Palace na Fulham wakitaka kutoa ofa zao kwa mchezaji huyo anayewekewa thamani ya pauni milioni 12 mwenye miaka 27 ambaye mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Nigeria. (Sun) Barcelona wanamfuatilia mshambualjia wa Everton raia Brazil Richarlison, 21. (Star) Kiungo wa kati wa kisosi cha Manchester City cha chini ya miaka 21 Phil Foden, 18, anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka sita. (Telegraph)
Chelsea wanataka kumuongezea mkataba wa miaka 12 mlinzi raia wa Brazil David Luiz, 31, baada ya msimu huu ambao utamwezesha kutafuta kwingine. (Mirror) Mlinzi wa kikosi cha chini ya miaka 21 wa Everton raia wa England Mason Holgate, 22, ameambiwa kuwa anaweza kuondoka kwa mkopo mwezi Januari. (Mirror) Marseille wanawatafuta mabeki wawili - Nacho Monreal, 32, wa Arsenal na Alberto Moreno, 26 wa Liverpool wakati wanapanga kuboresha kikosi chao mwezi Januari. (France Football, via Mirror)
Arsenal wanataka kumsaini wing'a wa Barcelona Mfaransa Ousmane Dembele lakini mshambuliaji Lionel Messi anasema Barcelona wanamtaka mchezaji huyo wa miaka 21. (Football.London) Liverpool bado wanaweza kumdsiania Dembela ikiwa watakuabaliani na bei ya Barcelona. (El Confidencial, via Star) Bournemouth wanataka kumtafuta kiungo wa kati wa Celtic na Scotland Callum McGregor, 25. (Scottish Sun) Meneja wa Everton Marco Silva anasema kiungo wa kati Morgan Schneiderlin bado ana matumaini ya siku za usoni kwenye klabu hiyo licha ya kukosa kucheza wiki za hivi karibuni. (Liverpool Echo) Mlinzi wa West Ham Reece Oxford, 19, alitazamwa na maajenti kutoka Manchester City, Borussia Dortmund na Hoffenheim wakati wa mechi ya hivi majuzi ya kikosi cha chini ya miaka 23. (Sun) Kocha wa Ujerumania Joachim Low amekiri kuwa muda wake katika timu hiyo ya taifa unafikia mwisho na anaweza kukubali fursa ya kuongoza Real Madrid (Marca)
Reading wamefanya mawasiliano na klabu ya Ureno ya Vitoria de Guimaraes, ambayo kocha wake amehusishwa na klabu hiyo. (Sky Sports) Mlinzi Muitalia Matteo Darmian anasema anajivunia kuwa mchezaji wa Mancheter United lakini amekosa sana kuwa na Italia na Seriea A. Juventus, Inter Milan, Napoli na Roma wote wanaripotiwa kutaka kumsani mchezaji huyo wa miaka 29. (Gazzetta dello Sport, via Sun) Tottenham wanastahili kutambuliwa kuwa klabu ambayo inaweza kushinda Premier League msimu huu, kwa mujibu wa mchezaji wa zamani Ryan Mason. (Talksport)

Post a Comment

0 Comments