we bring music and news for life


 

TRENDING

2018/12/08

Yajue Haya kuelekea Mchezo kati ya Chelsea vs Man City

Mchezo wa ligi kuu England kati ya Chelsea dhidi ya Manchester City, mchezo huu ambao ulikuwa unasubiria kwa hamu duniani na mashabiki mbali mbali wakiamini soka la kuvutia kwa pande zote mbili Huu mchezo utakuwa mgumu sana naamini kila timu itacheza open game kwa maana ya kushambulia na kutengeneza nafasi za mabao. Ukiangalia hizi timu kwenye msimamo wa ligi kuu England tunapata taswira msimu huu kila timu imecheza michezo 15 City, amekusanya alama 41 ameruhusu mabao 7 na wamefunga mabao 45
Katika idara ya ulinzi imekamilika zaidi muunganiko wa Laporte, na Stones, tunaiona ngome hiyo kuwa ngumu kupita wana uwezo mzuri kwa kutengeneza hata nafasi za mabao. Ukiangalia Chelsea,msimu huu mpaka sasa amevuna alama 31 pia wameruhusu wamefunga mabao 31 na wameruhusu mabao 13 tunaiona safu ya ulinzi ya Chelsea, msimu huu aipo vizuri ukimuangalia vizuri David Luiz, na Rudiger, ni wazuri wakiwa na mpira ila kwenye kutengeneza nafasi ndo shida ipo hapo pia sio wazuri kwenye kukaba hii inaleta kuwaletea madhara kuelekea mchezo huu. Leo nilimsikia kocha wa klabu ya Chelsea, akizungumza na waandishi wa habari akisema ” kila ninapokutana na Pep, nimekuwa napoteza mechi mbele yake huku pia akisisitiza kuwa sijui nitapataje ushindi”,.
Inaonekana wazi Sarri, ameshakubali matokeo kabla ya mechi na anaenda kukamilisha ratiba pengine hili pia hata wachezaji wanajiskiaje katika klabu. . . Mchezo huu me binafsi naona unaenda kuamuliwa eneo la kiungo Manchester City, katika safu hiyo wamekamilika zaidi wana viungo wabunifu wenye kasi na hata kufunga mabao Berndo ,Silva Fernandinho, wote wana uwezo na ligi pia msimu huu wameonyesha kiwango kikubwa zaidi. . . Ukiangalia Chelsea, idara hiyo wapo vizuri ila sasa kuna mambo ambayo Sarri, anashindwa kuelewa sina maana ya kuwa nimezidi hapana naeka mawazo yangu kuelekea mchezo huu kwa nini?Kante asimcheze kiungo wa kati mkabaji kwa maana ya kufanya battle na Fernandinho, kwenye kuwania mpira kwa sababu kama atampanga Jorginho, ni mchezaji mzuri ila amekosa nguvu na speed ni mzuri kwenye kupiga pass tuu kama atafanikiwa kuzuiliwa na Fernandinho, basi nafikiri Chelsea watakuwa kwenye wakati mgumu.

No comments:

Post a Comment

Pages