MISRI MWENYEJI AFCON 2019


Misri itaandaa fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon) 2019, Shirikisho la Kandanda Barani Afrika (Caf) limetangaza. Misri imewapiku Afrika Kusini kwa kura 16 kwa moja na mtu mmoja akishindwa kupiga kura katika mkutano wa kamati ya utendaji ya Caf uliofanyika nchini Senegal. Nchi ambayo ilitakiwa kuandaa fainali hizo ni Kameruni lakini hata hivyo walipokonywa nafasi hiyo mwezi Novemba kutikana na maandalizi kuwa na mwendo wa pole na usioridhisha. Misri sasa ina miezi sita tu kujiandaa na michuano hiyo ambayo kwa mara ya kwanza itahusisha timu 24 na kuanza kutimua vumbi mwezi Juni. Arsenal wakabidhiwa Man Utd Kombe la FA Wolves wazidi kushangaza miamba, wawalaza Liverpool Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 08.01.2019 Hii itakuwa mara ya tano kwa Misri kuandaa mashindano hayo. Mara ya mwisho kwa Mafarao hao kuandaa ilikuwa mwaka 2006 ambapo kombe lilibaki nyumbani. "Niishukuru Kamati ya Utendaji (ya Caf) kwa kutuamini, na pia naishukuru serikali kwa mchango wake mkubwa," amesema Rais wa Chama cha Kandnda cha Misri (EFA) Hany Abu Rida. "Tuliandaa mashindano haya mwaka 2006 na hiyo inatupatia changamoto ya kuandaa mashindano bora zaidi, na tupo tayari kuitekeleza kwa vitendo heshima hiyo." "Uhakika tuliopatiwa kutoka kwa serikali umetusaidia pakubwa kuwapiku Afrika Kusini na hilo litatufanya kuandaa mashindano bora kabisa," ameongeza Ahmed Shobair, Makamu Rais wa EFA. "Mashabiki watajitokeza tena viwanjani, na watajaza viwanja mpaka mwisho wa mashindano naahidi hilo." Misri itatumia viwanja nane kuandaa mashindano hayo vilivyopo kwenye majiji matano tofauti: Alexandria, Ismailia, Port Said, Suez na mji mkuu wa Cairo.
Mshambuliaji nyota wa Misri Mohammed Salah anatazamiwa kutetea taji lake la Mchezaji Bora wa Mwaka wa Afrika katika hafla itakayofanyika baadae hii leo. Uamuzi wa leo wa Caf umetangazwa katika mji mkuu wa Senegal wa Dakar ambapo baadae usiku kutafanyika sherehe za tuzo za mwaka za Caf. Mshambuliaji nyota wa Misri Mohammed Salah anatazamiwa kutetea taji lake la Mchezaji Bora wa Mwaka wa Afrika, achuana katika kuwania tuzo hiyo na Mgaboni Pierre-Emerick Aubameyang na Msenegali Sadio Mane. Baada ya Caf kuwafutia Kameruni uandalizi wa mashindano hayo, imewapa fursa ya kuandaa tena baada ya miaka miwili. Hali hiyo inamaanisha nchi zilizopangwa kuandaa mashindano hayo kwa mwaka 2021 na 2023 wameombwa kupeleka mbele. Ivory Coast, ambao walitakiwa kuandaa mashindano ya 2021, tayari wameshakata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo. Shirikisho la Mpira la Guinea limetangaza jana Jumatatu kukubali kupeleka mbele maandalizi yake ya Afcon kutoka mwaka 2023 mpaka 2025.

Post a Comment

0 Comments