Mohamed Salah: atawazwa mchezaji bora wa mwaka Afrika wa Caf kwa mwaka 2018


Mshambuliaji wa Misri na klabu ya Liverpool ya England Mohamed Salah ndiye Mchezaji Bora wa Mwaka wa Shirikisho la Soka Barani Afrika kwa mwaka 2018 - hii ikiwa ni mara yake ya pili kushinda tuzo hiyo. Salah, 26, alimshinda mwenzake wa Liverpool Sadio Mane kutoka Senegal na mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang. Alikabidhiwa tuzo hiyo katika sherehe iliyofanyika nchini Senegal Jumanne. "Nimekuwa na ndoto ya kushinda tuzo hii tangu nilipokuwa mdogo na sasa nimefanya hivyo mara mbili mtawalia," Salah alisema. Mshambuliaji wa Houston Dash kutoka Afrika Kusini Thembi Kgatlana alitawazwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa kike. Misri kuandaa fainali za Afcon 2019 Mo Salah mchezaji bora wa mwaka Afrika Salah apewa uraia wa heshima na kiongozi wa Chechnya Wenger awasifu wachezaji kutoka Afrika Salah pia alitawazwa Mwanakandanda Bora wa Mwaka wa Afrika wa BBC kwa mara ya pili mtawalia Desemba. Aliwafungia Liverpool mabao 44 msimu wa 2017-18 na kuisaidia klabu hiyo kufika fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ingawa walishindwa na Real Madrid. Aidha, alifunga mabao mawili akichezea Misri katika Kombe la Dunia nchini Urusi. Amefunga mabao 16 katika mechi 29 alizoichezea Liverpool mashindano yote msimu huu. Salah, Mane na Aubameyang wamo kwenye Kikosi Bora cha Mwaka Afrika pamoja na beki wa Manchester United Eric Bailly, kiungo wa kati wa Manchester City Riyad Mahrez, kiungo wa kati wa Liverpool Naby Keita na beki wa kushoto wa Tottenham Serge Aurier. Jumanne, Caf ilitangaza pia kwamba Misri itakuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Taifa Bingwa Afrika mwaka 2019 baada ya Cameroon kushindwa kujiandaa kwa wakati. Kikosi Bora cha Afrika XI: Denis Onyango (Mamelodi Sundowns/Uganda), Serge Aurier (Tottenham/Ivory Coast), Medhi Benatia (Juventus/Morocco), Eric Bailly (Manchester United/Ivory Coast), Kalidou Koulibaly (Napoli/Senegal); Naby Keita (Liverpool/Guinea), Thomas Partey (Atletico Madrid/Ghana), Riyad Mahrez (Manchester City/Algeria); Mohamed Salah (Liverpool/Misri), Pierre-Emerick Aubameyang (Arsenal/Gabon), Sadio Mane (Liverpool/Senegal

Post a Comment

0 Comments