Rashford ataumbua wengi sana By Privaldinho


Anakwenda kwa jina la Marcus Rashford kijana mzaliwa wa Jiji la Manchester alizaliwa 31/9/1997 mpaka sasa ana miaka 21. Hili ni zao la acardemy ya manchester united kwa asilimia 100%. Alijiunga na klabu ya manchester united akiwa na miaka 7 tu na alikuzwa hapo mpaka sasa tunamuona katika ligi kuu nchini England (Epl). Kijana huyuu alitambulishwa na Kocha Lous Van Gaal katika mashindano ya UEFA EUROPA LEGUE. Rashford alitajwa katika kikosi cha kwanza katika usiku wa ulaya na hii ni baada ya mshambuliaji Anthony Martial kupata majeruhi wakati wa mazoezi mepesi kuelekea mchezo wa siku hiyo uliokua kati ya Midtjylland. Hii ilikua ni mechi ya round ya 32 bora iliokua ya marudiano katika uwanja wa Old traford.
Katika siku hii rashford ilikua siku ambayo hajii kuisahau baada ya kufunga magoli mawili nakuisadia timu yake kupata ushindi wa magoli 5-1. Usiku huu ulimfanya Rashford kuvunja rekodi ya Gorge Best kua mchezaji mdogo kabisa kuwwahi kuifungia Manchester united ikiwa katika mashindano ya Ulaya. Siku tatu mbele Rashford aliaminiwa tena na kocha wake Louis Van Gaal na hii mechi ilikua dhidi ya Arsenal. Hii ndo ilikua mechi yake ya kwanza ligii kuu nchini England na katika mechi hii ilishuhudiwa Rashford akipiga magoli mawili mbele ya Cech na kutoa assist moja na kuifanya Manchester united kupata ushindi wa 3-2. Mechii hii ilimfanya Rashford kuandika Rekodi katika klabu yake na kua mchezaji wa tatu mwenye umri mdogo kuwahi kuifungia manchester united nyuma ya Federico Macheda na Danny Welbeck.
Tarehe 20/3/2016 hii siku ilikua ni siku ya Manchester derby ambayoo dunia nzima masikio na macho wanaangalia nini kitatokea katika mechi hiyo. Rashford aliaminiwa kuanza na alifanikiwa kufunga Goli moja tuu na ndo liliwapa ushindi katika mechi hiyo katika uwanja wa Etihad. Hii ilikua ni kwa mara ya kwanza kwa Manchester united kushinda katika uwanja huo tangu mwaka 2012. Akiwa na miaka 18 na siku 141 aliweka rekodi ya kua mchezaji mdogo zaidi kufunga katika manchester derby. Alimaliza msimu 2015 /2016 akiwa na magoli 8 ndani ya michezo 18 na bila kusahau alianza rasmi kucheza mwezi February 2016.
Msimu huo Rashford alifanikiwa kushinda tuzo ya Jimmy Murphy young player of the year akiungana na wachezaji kama Ryan Gigs, paul schoules, David Beckham na wengine wengi. Hii tuzo alipewa tarehe 30 May 2016. _______________________________________________ Msimu wa 2016/2017 timu ikiwa na kocha mpya Jose Mourinho Rashford alifanikiwa kuingia timu ya wa kubwa akipewa jezi namba 19. Alifanikiwa kufunga goli la kwanza katika msimu huo 27/8/2016 dhidi ya hull city. Rashford alifanikiwa kufunga goli katka nusu fainali mechi ya marudiano iliyofanyika Oldtraford dakika ya 107 na kuipa ushindi timu hiyo dhidi ya Anderlecht goli lililo ipeleka Manchester united Fainali ya Eurpa fainali iliyowakutanisha na Ajax. Rashford baada ya kusajiliwa kwa Ibrahimovic ilibidi abadilishwe namba na kuanza kucheza kama winger namba aliocheza katika kipindi chote cha kocha Jose mourinho. Pia huu ulikua msimu wa mafanikio sana kwake baada ya kufanikwa kushinda makombe matatu na kombe lake la kwanza kabisa ilikua ni EFL, na baadae Europa league na Community shield.
Huu msimu haukuwa msimu bora sana kwa rashford na hapa ndipo wachambuzi mbali mbali na mashabiki walipo mshushia lawama nzito kijana huyo na kumuona hafai. Ujio wa R.lukaku ndo ulizidi kudidimiza kipaji chake na hii ni baada ya lukaku kuaminiwa sana na mourinho na kumchezesha rashford winger kitu ambachoo yeye hua hapendezewi nacho. 2018/2019 kijana alirudi kujifua beach kwa nguvuu na kua na kiu ya kufanya vizuri lakini msimu huu ulikua tofautii ni rashford yupo vizuri ila morinho anazingua. Unajua ikawaje ? Rashford aliweza kupiga magoli mawili tuu akiwa chini ya mourinho msimu huu na mwanzoni mwa mwezi December akatangazwa mourinho kafukuzwa pale United.
Hapa ndipo rashford alizaliwa upya na hii nibaada ya kurudi wenye timu akiongozwa na Kocha wa muda Ole Gunnar Solskjaer. [1/18, 10:02 PM] Sativ: Mashabiki wa manchester united wao wanaita NEW MANCHESTER UNITED teh teh teh. Rashford alimkaribisha Ole katika ligi kuu kwa kufunga goli la kwanza dhidi ya Cardif huku united ikishinda magoli 5-1. Chini ya kocha Ole rashford alipangwa kama namba 9 mechi zote (6) na kumuweka R.lukaku nje. Na kuna maneno yanasemwa kua kocha huyo aliekuja kurudisha utamaduni wa Manchester united amesha mwambia Rashford kua kwa sasa yeye ndio chaguo lake namba moja katika safu ya ushambuliaji. Rashford wa hizi mechi sita anautofauti sana amecheza mechi 5 za ligi na kaweza kaweza kufunga magoli 5 na kutoa assist 4 . Huu mwaka kashafunga Goli 7 na kutoa assist 6 nKupelekea kuwa mchezaji aliekua na mchango zaidi nyuma ya paul Pogba .
Kwa mfumo anaoenda nao Ole ninaimani kubwa kua huyu Rashford ataumbua wachambuzi na mashabiki wengi wa soka kuna vitu vingii anavifanya sasa. Sasa anamiaka 21 zingatia umri wake na huyu ni Rashford wa Manchester united lakini yupo Rashford wa timu ya taifa ya England.

Post a Comment

0 Comments