Samatta amefungua milangoNani ni shujaa? Jitazame kwenye kioo utaona. Je? Nchi yaTanzania ukiiweka kwenye kioo ijitazame taswira yake inaonekana vipi?. Naamini kutakuwa na mashujaa kibao watao jitokeza katika taswira ya kioo angavu. Wanao ipeperusha bendera ya nchi. Mnamo mwaka 2010, MBWANA ALY SAMATA. Kipindi hiko alikua anakipiga katika klabu ya African Lyon ya jijini dare s salaam ambapo alipata umaarufu mkubwa kwa kazi aliyo kuwa akiifanya na ndipo Simba SC ikaamsajili, mnamo july 1 akajiunga na klabu hiyo. Alisajiliwa kama mchezaji mdogo wa akiba na kama silaha itakayo tumiwa hapo baadae. Hakuna aliyejua ipo siku Samatta angekuwa kinara wa mabao mbele ya wazungu tena kwenye ardhi yao.


TP Mazembe ya nchini Congo DRC ikamsajili. kwa kiasi cha 70€. Aliutumikia vyema mshahara mnono wa Moses Katumbi kwa miaka mitano. Wachezaji wa Kitanzania waliowahi kuwa wafungaji bora wa klabu bingwa tokea 2000. 1⃣ Mbwana Samatta – Magoli 7 – 2015 2⃣ Mrisho Ngassa – Magoli 6 – 2014 January 26 mwaka 2016 Samatta alijiwekea rekodi yake nchini Tanzania kwa kupata mkataba na KRC Genk ya nchini Ubelgiji inayocheza ligi ya kuu kwa dau la 1300€ kwa muda wa miaka miwili yaani mpaka 2018.


Lakini kwa juhudi na mafanikio aliyaleta klabuni hapo akaongezewa mkataba mpaka ifikapo mwezi june 2021. Kwa sasa Samatta ana umri wa miaka 26, uzito wa kilogramu 70 na urefu wa 179 cm. kwa msimu wa 2018/19 katika mechi 20 alizo cheza kafumania nyavu mara 15 na kumfanya awe kinara wa kufunga mabao wa muda katika ligi hiyo. Ana mabao 3 ya ligi ndogo ya mabingwa wa ulaya ‘EUROPA’. Hii inamfanya kuwa mchezaji anaetamanisha vilabu vya nchini ulaya vya usawa wa kati kumsajiri.


Klabu KRC Genk iliandaa makala ya Mbwana Aly Samata. Na katika makala hiyo namnukuu Samata “najikubali kwa kupiga hatua kubwa, kutoka nchini kwangu mpaka hapa nilipo”… aliongezea “ kutimiza moja ya ndoto zangu. Najisikia ni kama natengeneza njia kwa wenzangu kutoka Tanzania.” hii inamfanya kuwa chachu kwa vijana kama wanao chipukia mfano akina Chilunda Shaban wa Tenerife ya uhispania na Haji Mnoga wa Portsmouth ya uingereza. Mbwana anaendelea kushika tochi ya mpira kwa Tanzania na kupeperusha bendera ya Tanzania. Na hiyo ndiyo tafsiri ya shujaa. Mwandishi : ISACK MSINJILI