Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 10.01.2019: Ramsey, Morata, Milenkovic, Rice, Tarkowski, Koulibaly

Kiungo wa kati wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 28, amekubali kujiunga Juventus mwezi Juni mwaka huu. (Guardian) Atletico Madrid imeingia katika kinyang'anyiro cha kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Uhispania Alvaro Morata, 26. Kuna tetesi kuwa Morata huenda akajiunga na Sevilla. (Goal) Real Madrid wanajiandaa kutoa ofa ya euro milioni 9 kumenyana na mahasimu wao Manchester United katika juhudi za kumnunua mlinzi wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 27. (Il Mattino, via Talksport) Azma ya United ya kumnunua mlinzi wa Fiorentina na Serbia Nikola Milenkovic, 21, huenda imefifia baada ya Jose Mourinho kutimuliwa kutoka klabu hiyo. (ESPN) Burnley wanakadiria kuwa thamani ya mlinzi wa England James Tarkowski, 26 ni euro milioni 50 japo Liverpool wanapania kumchukua kiungo huyo kwa mkopo. (Sun) Mchambuliaji wa Southampton, mtaliano Manolo Gabbiadini, 27, amekubali kujiunga tena na Sampdoria kwa kima cha euro milioni 11.7. (Guardian)
Manolo Gabbiadini, mshambuliaji wa Southampton, Tottenham wanatafakari uwezekano wa kumsajili mlinzi wa Uswidi Joachim Andersen, 22, ikiwa beki wa kati wa Ubelgiji Toby Alderweireld, 29, atahama klabu hiyo. (Independent) Manchester City inapania kumsajili kiungo wa kati wa West Ham na Jamhuri ya Ireland Declan Rice, 19, kujaza pengo lililoachwa na mchezaji wa kimataifa wa Brazil Fernandinho, 33. (Sun) Ajenti wa mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata amekubali kufanya mazungumzo na vilabu viwili vya Uhispania kwa mujibu wa mtaalamu wa kandanda wa Ulaya Guillem Balague, lakini 'The Blues' huenda wasikubali kumuachilia nyota huyo wa miaka 26 kabla wampate mchezaji atakayechukua nafasi yake. (BBC Radio 5 live In Short) Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amemwambia kiungo wa kati wa klabu hiyo Denis Suarez 25, ambaye analengwa na Arsenal kuwa anaweza kuondoka Nou Camp. (Marca)
Denis Suarez (kushoto) Arsenal wanapania kumsajili kiungo wa kati wa Porto Hector Herrera, 28, kupitia uhamisho bila malipo msimu huu kuchukua nafasi ya Aaron Ramsey, ambaye makataba wake unaelekea kukamilika. (Tutto Mercato Web) Unai Emery ameidhinisha Arsenal kumsajili winga wa Ubelgiji Yannick Carrasco, 24, kutoka klabu ya Dalian Yifang inayoshiriki ligi kuu ya Uchina. (Foot Mercato) Liverpool wanajiandaa kukatiza uhamisho wa winga wa Wales Ben Woodburn ambaye amekuwa akiichezea Sheffield United kwa mkopo huku wakitafakari uwezekano wa kiungo huyo kujiunga na vilabu vya Blackburn Rovers, Brentford na Hull City. (Goal)
Ben Woodburn (kulia) Mshambuliaji wa West Ham, muingereza Andy Carroll, 30, anatafakari uwezekano wa kusalia katika klabu licha ya kuwa mkataba wake unakamilika mwisho wa msimu huu. (Sky Sports) Newcastle wameshinikizwa kuongeza ofa yao ikiwa wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Atlanta United na Paraguay Miguel Almiron, 24. (ABC Cardinal, via Guardian) Meneja wa Cardiff Neil Warnock amesafiri nchini Ufaransa katika harakati za kumsajili mshambuliaji wa Nantes Emiliano Sala, japo kuna tetesi nyota huyo wa miaka 28 raia wa Argentina hajafanya uamuzi. (Sun) Bora kutoka Jumatano Inter Milan wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Croatia Ivan Perisic, 29, kwa Manchester United ndipo waweze kupata pesa za kumnunua kiungo wa kati wa Real Madrid ambaye pia anatokea Croatia Luka Modric, 33. (Tuttosport, kupitia Calciomercato) Mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Mauro Icardi, 25, ni miongoni mwa wachezajia ambao mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich anataka kuwanunua mwezi huu. (Mirror)
Callum Hudson-Odoi alijiunga na Chelsea mwaka 2007 Bayern Munich wameongeza kitita ambacho wako tayari kutoa kumchukua mshambuliaji wa Chelsea Callum Hudson-Odoi hadi £35m. Mchezaji huyo wa miaka 18 amekariri hamu yake ya kutaka kuihama klabu hiyo ya Stamford Bridge mwezi huu. (Guardian) Chelsea wanamtaka mshambuliaji wa AC Milan kutoka Ureno Andre Silva - ambaye yupo Sevilla kwa mkopo - lakini uhamisho huo utategemea the Blues kukubali mshambuliaji wao wa Uhispania Alvaro Morata ahamie klabu hiyo ya Sevilla. (Sun) Crystal Palace wanamtaka mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham ajiunge nao kwa mkopo baada ya mchezaji huyo wa miaka 21 ambaye kwa sasa yupo Aston Villa kwa mkopo kukataa fursa ya kujiunga na Wolves. (Mirror)
Tammy Abraham Everton wanamnyatia kiungo wa kati wa Porto na Algeria Yacine Brahimi na walimtuma skauti kumfuatilia Jumatatu wakati wa mechia ambayo walishinda 3-1 dhidi ya Nacional. Kiungo huyo wa miaka 28 alifunga mabao mawili mechi hiyo. (Mirror) Fulham waliwatembeza beki wa England Gary Cahill, 33, winga wa Nigeria Victor Moses na kiungo wa kati wa England Danny Drinkwater, wote wawili wakiwa na miaka 28, katika uwanja wao wa mazoezi katika juhudi za kutaka kuwashawishi kujiunga nao kutoka Chelsea. (Love Sport Radio)