Adrien Silva achoshwa na kusalia benchi klabuni Leicester Kocha mpya wa klabu ya Stoke Nathan Jones anataka kukipa nguvu mpya kikosi chake kwa kukaribisha ofa za timu zinazowataka wachezaji wake wakongwe watatu - Bojan, Darren Fletcher na Peter Crouch - ambao ndio wanaopokea malipo makubwa Zaidi klabuni hapo. (Daily Mail)
Mshambuliaji mkongwe Peter Crouch akalia kuti kavu klabuni Stoke. Beki wa West Ham Reece Oxford, 20, anatakiwa na kocha Martin O'Neil wa klabu ya ligi ya daraja la kwanzaya Nottingham Forest, klabu hiyo imetenga kitita cha pauni milioni 8 ili kumnasa kinda huyo. (Mirror) Oxford tayari ameshacheza kwa mkopo katika ligi ya Ujerumani, Bundesliga, na klabu ya Eintracht Frankfurt pia wameonesha nia ya kumsajili karika dirisha la usajili la mwezi huu. (Sky)
Ben Woodburn anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji goli mdogo zaidi katika historia ya Liverpool Ben Woodburn, 19, ambaye ni mchezaji anayeshikilia rekodi ya kufunga bao akiwa na umri mdogo zaidi katika historia ya Liverpool anaweza kujiunga na klabu ya Hull kwa mkopo baada ya kumaliza muda wake wa mkopo na Sheffield United. (Daily Mail)
No comments:
Post a Comment