BREAKING: Mshambuliaji wa Cardiff aliyepotea na ndege amefariki dunia


Baada ya sintofahamu kwa zaidi ya wiki kadhaa kuhusiana na wapi walipo mshambuliaji mpya wa Cardiff City Emiliano Sala na rubani wake David Ibbston baada ya ndege yao ndogo walioyokuwa wanasafiria kutoka Nantes kurudi Cardiff kupotea January 21 ikiwa katika pwani ya Guensney. February 6 ziliripotiwa taarifa baada ya uchunguzi binafsi kufanyika walibaini kuwa ndege hiyo imeanguka na kuzama bahari, hivyo walibaini mwili mmoja waliyokuwa wameukuta katika mabaki ya ndege hiyo chini ya bahari ila wakawa hawajafanikiwa kuugundua na kuupeleka mahabara.
Baada ya uchunguzi wakina kufanya imebainika kuwa mwili ule ni Emiliano Sala na bado mwili wa rubani wake unaendelea kutafuta, polisi wa Dorset wamethibitisha kuwa Emiliano Sala amefariki dunia, Sala amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 29 (1990-2019) hiyo ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kusaini Cardiff City akitokea Nantes FC ya Ufaransa kwa uhamisho wa pound milioni 15.

Emiliano Sala na rubani wake aliyepa nae ajali