BREAKING: Watu 8 waliochoma Kituo cha Polisi wamehukumiwa kukaa jela maisha


Leo February 22, 2019 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu kifungo cha maisha jela washtakiwa 8 kati ya 18 baada ya kutiwa hatiani katika kesi ya kuchoma moto Kituo cha Polisi cha Bunju A. Jumla ya washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni 35 ambapo awali Mahakama ilikwisha waachia huru washtakiwa 17 na kubaki 18 ambapo 8 ndio wametiwa hatiani leo huku 10 wakiachiwa huru. Washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na makosa 6 ikiwemo kuchoma kituo hicho moto ambapo wanadaiwa walilitenda Julai 10, 2015. Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amesema kitendo walichofanya washitakiwa ni unyama kwa kuchoma moto kituo hicho.

 WALIOCHOMA MOTO KITUO CHA POLISI, WAKISUBIRIA HUKUMU