FIFA imeifungia Chelsea kufanya usajili wa wachezaji


Club ya Chelsea ya England leo imekumbana na adhabu ya kufungiwa kufanya usajili na shirikisho la soka la kimataifa FIFA kwa kukiuka sheria za usajili. FIFA imeifungia Chelsea kufanya usajili wa kwa kipindi cha usajili wa madirisha mawili, baada ya kubainika kuwa wamefanya usajili wa wachezaji wenye umri chini ya miaka 18 kama ambavyo sheria zinataka. Chelsea wamekumbana na adhabu hiyo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina kudaiwa kuwa walimsajili staa wa Burkinafaso Bertrand Traore akiwa na miaka 16 mwaka 2017, adhabu ya Chelsea imeambatana na faini ya pound 460000 huku FA pia wakipigwa faini ya pound 390000.