RAMSEY ASAINI MAKUBALIANO YA KUJIUNGA NA JUVENTUSKiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey ametia saini makubaliano ya awali ya kujiunga na klabu ya Juventus msimu ujao kwa katika cha pauni £400,000 kwa wiki. Nyota huyo wa miaka 28 amekubali mkataba wa miaka minne utakaomwezesha kujiunga na ligi ya champions ya Italia bila malipo baada ya kuwa Arsenal kwa miaka 11. Ramsey alifuzu sehemu ya kwanza ya uchunguzi wa kimatibabu mwezi Januari, na kuchagua Juve baada ya kushauriana na wadau kadhaa wa klabu hiyo. Atakuwa mchezaji wa Uingereza anayelipwa mshahara mkubwa. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales unakamilika Juni 30 na Gunners hawatapokea malipo yoyote atakapo ondoka. Ikithibitisha mpango huo, Juventus imesema italipa ada ya pauni milioni £3.2 lakini haikuelezea ada hiyo ni ya nini. Arsenal imesema mchango wa Ramsey ulikuwa mkubwa sana katika klabu hiyo na kuongeza kuwa "atakasalia katika kumbu kumbu ya historia" ya mashabiki. Akiandika katika mtandao wake Instagram, Ramsey aliwashukuru mashabiki wa Arsenal na kusema kuwa"ataendelea kuwaunga mkono 100%". Aliendelea kuandika : "Mlinikaribisha katika klabu hiyo nikiwa kijana mdogo na nimeshuhudia nyakati nzuri na mbaya. "Nasikitika kuondoka baada ya miaka 11 ya ufanisi sijui nielezee vipi hisia zangu muda huu. Asanteni." Charles, Rush, Ramsey...

Juventus wamemkaribisha rasmi Ramsey katika mitandao yao ya kijamii Tuvuti ya Juventus imemkaribisha Ramsey kwa kuandika kwamba atakuwa mkazi wa Wales wa tatu kuiwakilisha klabu hiyo baada ya John Charles na Ian Rush. Ramsey, alijiunga na Arsenal akitokea Cardiff City mwaka 2008 kwa ada ya £4.8m, pia aliwahi kufanya mazungumzo na Barcelona na kupokea ofa kutoka klabu ya Paris St-Germain. Bayern Munich, Inter Milan na Real Madrid walionesha nia ya kutaka kumnunua kiungo huyo, huku mshambuliaji wa Real Gareth Bale akidaiwa kumshauri kuungana nae katika ligi kuu ya Uhispania. Arsenal ilimpatia Ramsey ofa ya mkataba mpya mwezi Septemba lakini hatua hiyo ilipingwa na wakuu wa klabu ambao hawakuwa tayari kugharamia mshahara wake mkubwa. Kocha mkuu Unai Emery anatilia shaka jukumu la Ramsey katika kikosi chake. Ramsey alitaka kucheza namba nane hatua ambaye ilikuwa inakinzana na maono ya Emery. Amechezea Arsenal mara 259, na kufunga mabao mara 61. Wachezaji wanazungumziaje hatua ya Ramsey


Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya England Ian Wright kupitia BBC Radio: Sidhani Aaron Ramsey angelikataa ofa kama hiyo kutoka kwa vilabu vinavyohitaji huduma zake. Ukizingatia mikataba aliyopewa, Arsenal haingeliweza kuendelea kumlipa sawa na wachezaji wake wengine. Nakumbuka Arsene Wenger alisema matukio kama hayo yatakua ya kawaidi. Wachezaji wanapewa ofa kubwa kiasi cha wao kudhubuti kuvunja mikataba waliyo nayo. Katika umri huu, dhamani yake ni angalau £30-40m. Juventus wanaweka akiba ya fedha nyingi hata baada ya kumlipa kitita hicho kikubwa. Ni hatua ambayo mtu yoyote hatachelea kuchukua isipokuwa klabu anayotoka. Mshambuliaji wa zamani Blackburn Chris Sutton: Arsenal wamefanya makosa kuwaachia wachezaji mwanya wa kutengua mikataba yao. Zama zetu, unapewa mkata mwingine ukisalia na miaka miwili kabla ya mkataba wako kukamilika, ikiwa klabu inathamini mchango wako. Arsenal wamejipalia wenyewe makaa ya moto.