Hudson-Odoi, wa kati
Winga Willian, 30 wa Chelsea na Brazil, anataka kusaini mkataba wa miaka mitatu, lakini kuna tetesi amepewa mkataba wa mwaka mmoja. (Sport Witness) Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini alitaka kumsaini mchezaji wa zamani wa Cardiff, Gary Medel mwezi Januari lakini juhudi zake zilitibuka baada ya Besiktas kuitisha ada ya uhamisho. (Talksport) Meneja wa Inter Milan Luciano Spalletti anaamini Arsenal "walimlaghai" winga wa Croatia Ivan Perisic, 29, katika pendekezo la uhamisho wa Januari. (Rai Sport via Independent)
Tiemoue Bakayoko,
kushoto Kiungo wa kati wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 24, ambaye yuko AC Milan kwa mkopo kutoka Chelsea, amesema angependelea kusalia katika klabu huyo ya Italia. (Corriere dello Sport via Four Four Two) Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anahofia mlinzi wake Joe Gomez,21 huenda akahitaji kufanyiwa upasuaji. (Liverpool Echo) Newcastle wanajianda kutangaza kuondoka kwa kocha wao wa zamani Peter Beardsley ambaye alikua mkufunzi wa timu ya wachezaji wa chini ya miaka -23. (Mail)