Luka Modric ; Hakuna wa kuziba pengo la Ronaldo


Kiungo wa kimataifa wa Croatia anayeichezea Real Madrid ya Hispania Luka Modric ameweka wazi kuwa baada ya kuondoka kwa Cristiano Ronaldo hakuna wa kuziba pengo lake, maneno hayo Luka Modric ameyaongea wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wa maruadiano wa 16 bora ya UEFA Champions League dhidi ya Ajax March 5 2019.

 Kauli hoyo ya Luka Modric inakuja ikiwa ni siku chache zimepita toka timu hiyo ishindwe kupata matokeo katika mchezo wa El Clasico dhidi ya wapinzani wao wakuu nchini Hispania club ya FC Barcelona, ambapo wametolewa katika michezo ya Copa del Rey na kuongeza tofauti ya point 12 katika LaLiga dhidi ya Barcelona wanaoongoza Ligi.


Cristiano Ronaldo aliondoka Real Madrid na kujiunga na Juventus mwezi July 2018 baada ya kudumu na Real Madrid kwa miaka 9, baada ya kuondoka Real Madrid walifanya usajili wa washambuliaji wawili kama Vinicius Junior na Mariano Diaz ambao wote wameshindwa kuwa mbadala wa Ronaldo ambaye ndio mfungaji bora wa muda wote Ulaya.

 “Kukosekana kwa Ronaldo nafikiri kila timu lazima itahisi kukosekana kwake kutafuta mbadala wa Cristiano Ronaldo kwa sasa kiukweli haiwezekani, kwa alichotufanyia katika hii club kiukweli tunamkumbuka, club inahitaji wachezaji wengine ambao wataweza kufanya alichoifanyia Real Madrid, Cristiano Ronaldo anafunga magoli 50 huwezi kumpata mwingine aliyefanya hivyo”>>>Luka Modric