Arsenal ina hamu ya kumsajili mchezaji wa Ajax Nicolas Tagliafico, mwenye umri wa miaka 26, au mlinzi wa Celtic na timu ya Scotland Kieran Tierney, mwenye umri wa miaka 21, kuichukua nafasi ya beki wa kushoto wa Uhispania Nacho Monreal, iwapo mchezaji huyo wa miaka 33 ataondoka Barcelona. (Mirror)
Manchester United na Liverpool zote zina hamu ya kumsajili mchezaji wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 26mchezaij wa kiungo cha kati Isco. (Tuttosport)
Meneja mpya wa Leicester Brendan Rodgers anataka kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Aston Villa John McGinn, mwenye umri wa miaka 24. (Birmingham Mail)
Liverpool imehusishwa na mshambuliaji wa RB Leipzig na timu ya taifa ya Ujerumani Timo Werner, licha ya hamu kutoka kwa Bayern Munich kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Liverpool Echo)
Arsenal inataka kumsajili winga wa Ubelgiji Yannick Carrasco, mwenye miaka 25, kutoka timu ya Uchina, Dalian Yifang, baada ya kushindwa kupata mkataba wa mkopo katika dirisha la uhamisho la Januari. (Express)
Uhamisho wa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Wales Gareth Bale umeshuka thamani hadi £63m, kumaanisha Real Madrid inaelekea kupata hasara ya £30m iwapo watamuuza mchezaji huyo wa miaka 29 katika msimu wa joto. (Mirror)
Jamie Carragher anasema klabu yake ya zamani Liverpool bado inahitaji kutafuta mchezaji atakayeichukua nafasi ya mchezaji wa kiungo cha kati mshambuliaji Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 26, aliyelekea Barcelona mnamo Januari 2018. (Mirror)
Mashabiki wa Arsenal wanaweka shinikizo kwa klabu hiyo kumuita Calum Chambers, mwenye miaka 24, kutoka kwenye mkataba wake wa mkopo huko Fulham, huku mlinzi huyo aliyegeuka kuwa mshambuliaji akiridhisha timu hiyo ya Cottagers msimu huu. (Express)
Aliyekuwa mlinzi wa Manchester City Joleon Lescott hafikiri mchezaji wa kiungo cha kati Phil Foden, mwenye miaka 18, anastahili kuondoka Etihad kwa mkopo. (Manchester Evening News)
Meneja wa England Gareth Southgate anafikiria kumsajili winga wa Crystal Palace Andros Townsend, mwenye umri wa miaka 27, katika kumuita upya kuichezea timu ya taifa mwezi huu. (Mirror) Aliyekuwa Meneja wa Hull, Aston Villa, Wigan, Sunderland na kwa sasa Sheffield, Steve Bruce amefichua kwamba alitambuliwa kuugua saratani mnamo 2017.(Telegraph)