Ligi kuu England Golden Boot: Salah, Mane na Aubameyang watuzwa pamoja


Sadio Mane na Pierre-Emerick Aubameyang wafunga mabao ya fanali na kufanikiwa kutuzwa kwa pamoja na Mohamed Salah wafungaji mabao bora katika ligi kuu ya England.

 Mabao mawili aliyofunga Aubameyang katika mechi ya Arsenal dhidi ya Burnley imemaanisha amepata kujiunga na Salah na chezaji mwenzake wa Liverpool Mane, aliyeitinga Wolves, kwa mkusanyiko wa mabao 22.

 Salah alishinda tuzo hiyo msimu uliopita.


 Ni ushindi wa chini wa taji hilo tangu 2010-11, wakati Dimitar Berbatov na Carlos Tevez waliposhinda pamoja tuzo hiyo ya Golden Boot inayopewa mfungaji mabao mengi kila mmoja akiwa amefunga mabao 20.

 Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Gabon Aubameyang aliyefunga mara mbili baada ya kipindi cha mapumziko huko Turf Moor amesema: "Napokea taji hili na wachezaji wengine wawili ninaowapenda, g wachezaji bora na Waafrika. Tunaiwakilisha Afrika, ni vizuri.

 "Ninafurahi tumeshinda, na napokea tuzo hii [Golden Boot] tna watu nnaowapenda. wachezaji wenzangu walijua kuhusu tuzo hii. Mimi sikusema kitu. Sikutaka wacheze wakinilenga mimi. Mimi napneda kushirikiana na wenzangu."

Salah amekuwa mchezaji wa sita kushinda taji hilo la Golden Boot katika misimu inayofuatana'Wote ni wachezaji wangu'

 Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ameeleza mshtuko na furaha kwa mchezaji huyo wa zamani wa kiungo cha mbele wa Dortmund aliyemsajili kutoka Saint-Etienne mnamo 2013, alipokuwa anakiongoza kikosi huko Westfalenstadion.

 "Auba pia? wapewa tuzo tatu? Ni vizuri. wote ni wachezaji wangu" amesema. Salah, mwenye umri wa miaka 26, amefunga mabao 32 msimu uliopita. Idadi hiyo ni rekodi ya mabao mengi zaidi katika kampeni ya mechi 38.

 Amekuwa mchezaji wa sita kushinda taji hilo katika misimu inayofuatana. Harry Kane wa Tottenham mchezaji wa mwisho kulizuia taji hilo la ligi kuu ya Engalnd baadaya kulishinda mnamo msimu wa 2015-16 na 2016-17, alimaliza kwa mabao 17 baada ya kujruhiwa katika msimu.