Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 11/05/2019: Sancho, De Ligt, Hazard, Maguire, Ozil


Mshambuliaji wa Chelsea Ubelgiji Eden Hazard, 28, yuko katika harakati ya kukubali masharti mapya na Real Madrid kuhusiana na uhamisho mwisho wa msimu huu . (Independent)

Manchester United ilikosa fursa muhimu ya kumsaini nahodha wa klabu ya Ajax na uholanzi Matthijs de Ligt, 19, kwa kuwa iliambiwa kwamba mchezaji huyo atakjuwa mnene kupitia kiasi. (Mirror) Winga wa Uingereza Jadon Sancho, 19, atasalia katika klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund mwisho wa msimu huu na kupinga kurudi katika ligi ya Uingereza. (Sun)


Man United itamwachilia beki wa Ivory Coast Eric Bailly kujiunga na Arsenal - iwapo klabu hiyo itamuuza kwa dau la £30m walilolipa kununua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 2016. (Metro)

Beki wa Leicester na Uingereza Harry Maguire huenda akaichezea klabu yake mechi yake ya mwisho siku ya Jumapili. Tottenham, Arsenal, Chelsea na Manchester United wote wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 , lakini Leicester hawatamuuza kwa dau la chini ya £60m. (Sun)

Manchester United ina hamu ya kumsaini winga wa Swansea Daniel James. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 raia wa Uingereza pia amevutia hamu klabu kama vile Everton, Newcastle na Leeds. (ESPN)


Kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil "anatoka damu ya Arsenal" na atasalia katika klabu hiyo ya Uingereza hadi 2021, ajenti wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amesema.. (Independent)

Kiungo wa kati wa Real Madrid Marcos Llorente anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya La Liga mwisho wa msimu , huku baadhi ya klabu za ligi ya Uingereza zikiwa na hamu ya kumsainraia huyo wa Uhispania. (ESPN)

Arsenal ni mojawapo wa klabu zinazotaka kumsaini Llorente. (AS - in Spanish). Tottenham inatarajiwa kumsaini kiungo wa kati wa Bolton, 18, Luca Connell . (Sun)


Uhamisho wa kiungo wa kati wa Man Utd na Ufaransa Paul Pogba kuelekea Real Madrid huenda usifanyike , baada ya ajneti wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 Mino Raiola kupigwa marafuku ya miezi mitatu kutowakilisha wachezaji. (Talksport)

Kipa wa Burnley Joe Hart, 32, natarajiwa kuondoka katika ligi ya Premia baada ya msimu mmoja mwisho wa msimu huu lakini mshambuliaji Peter Crouch, 38, anatarajiwa kusalia .

(Mirror) Afisa mkuu wa zamani wa klabu ya Arsenal na afisa mkuu mtendaji wa AC Milan Ivan Gazidis anataka kumleta beki Shkodran Mustafi nchini Itali. Gazidis alimleta Mustafi, 27, katika klabu ya Arsenal 2016. (Tuttosport via Metro)


West Ham itawauza wachezaji sita ikiwemo mshambuliaji wa Uhispania Lucas Perez, 30, na beki wa Uingereza mwenye umri wa miaka 20 Reece Oxford kama miongoni mwa wachezaji inaotaka kuimarisha kikosi chake. (Evening Standard)

Mkufunzi wa Everton Marco Silva anasema kuwa ana matumaini ya kumsaini kwa mkopo kiungo wakati wa Barcelona kwa mkopo Andre Gomes kwa mkataba wa kudumu.Mchezaji huyo wa Ureno ,25, amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Tottenham. (Liverpool Echo)

Mkufunzi wa zamani wa Leicester Claudio Ranieri anasema kuwa atajiuzulu kama mkufunzi wa Roma mwisho wa msimu huu . (Goal)