Tetesi za soka Ulaya Jumanne 07.05 2019


Haki miliki ya picha Reuters Kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba, 26, anafikiria kuhamia Real Madrid mwisho wa msimu , lakini matumaini yake ya kuhamia klabu hiyo yatategemea Man United kupunguza thamani yake ya £160m. (Telegraph)
 Pogba atalazimisha kuondoka hata iwapo Man United itakataa kumuuza. (ESPN)
 Manchester City inakaribia kuingia makubaliano na kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, huku klabu hizo zikijadiliana kuhusu dau la kati ya £50m na £60m kwa mchezaji huyo wa Portugal mwenye umri wa miaka 24. (Sky Sports)


Beki wa Ajax Matthijs de Ligt, 19, amekataa uhamisho wa kuelekea Manchester United wenye thamani ya £60m. (Star)
 Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amejiunga katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Brazil na Ajax David Neres kwa dau la £35m . (Sun)
 Manchester United iko tayari kuanza uhamisho wa wachezaji inaowalenga ili kuimarisha kikosi hicho na tayari imewasiliana na Juventus kuhusu kumsaini mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala kwa dau la £85m(Calciomercato, via Mail)


Tottenham na Everton wanamuwania mshambuliaji wa Real Betis Giovani Lo Celso, 23. (Sun) Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29, ameambiwa kwamba hatakikani katika klabu ya Real Madrid katika mkutano wa ana kwa ana na mkufunzi Zinedine Zidane, lakini bado anataka kusalia katika klabu hiyo . (Mail)
 Mkufunzi wa Napoli na aliyekuwa mkufunzi wa zamani wa Chelsea Carlo Ancelotti ametoa ishara za kutaka kumsajili winga wa Mexico Hirving Lozano, 23, ambaye amehusishwa na uhamisho wa Manchester United. (Calciomercato)


Ancelotti amekataa kupiga madai ya kutaka kumsajili beki wa Tottenham Kieran Trippier, 28, baada ya mke wa mchezaji huyo wa Uingereza kuonekana akitafutia shule watoto wake mjini Napoli.. (Talksport)
 Winga wa Ufaransa Anthony Martial, 23, anakabiliwa na changamoto ya kumshawishi mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer kwamba ana kandarasi ya muda mrefu katika klabu hiyo.. (Mail)
 Solskjaer atasikiliza kuhusu ofa za Martial zitakazowasilishwa kutokana na tabia yake mbaya wakati wa mazoezi.. (Sun)
 Maajenti wa Martial wameandika katika mtandao wa instagram ili kutetea rekodi ya mshambuliaji huyo wa Man United huku kukiwa na ukosoaji kuhusu kiwango cha mchezo wa uwanjani Old Trafford.(Manchester Evening News)


Mkufunzi wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger, 69, amekataa ofa nyegine ya pili kuifunza klabu ya Fulham, baada ya kukataa kwa mara ya kwanza mnamo mwezi Novemba kabla ya kumuajiri Claudio Ranieri.. (Mail)
 Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Antonio Conte anasema kuwa kuna asilimia 60 kwamba huenda akarudi kufunza katika ligi ya Serie A msimu ujao.. (Le Iene - in Italian)
 Newcastle United imekuwa ikimchunguza kiungo wa kati wa Uingereza na Coventry Tom Bayliss, 20, kabla ya kumsajili mwisho wa msimu huu . (Chronicle)
 Kipa wa Poland Marcin Bulka, 19, anatarajiwa kuondoka Chelsea mwisho wa msimu huu na atatia saini kandarasi ya mapema na Paris Saint-Germain. (Goal.com)
 Beki wa zamani wa Uingereza Gary Cahill, 33, ambaye anaondoka Chelsea mwisho wa msimu huu , anasema hajaridhika na soka ya kiwango cha juu na anasisitiza anaweza kuendelea kucheza. (Talksport)
Tottenham inajiandaa kucheza msimu ujao bila ya kiungo wa kimataifa wa Denmark kiungo Christian Eriksen, 27, na wanaelekea kumsajili kiungo wa Ajax Donny Van de Beek 22, ambaye pia anatakiwa na Real Madrid na Bayern Munich.(Mirror )
 Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri ameitaka klabu yake kumsajili moja kwa moja mshambuliaji Gonzalo Higuain ambaye anaichezea Chelsea kwa mkopo akitokea Juventus ili kuimarisha kikosi chake. (Goal.com)


Mchezaji wa kimataifa wa England Danny Welbeck, 28 hatopewa mkataba mpya na klabu yake ya Arsenal na ataondoka akiwa mchezaji huru katika dirisha lijalo. (Sky Sports)
 Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane atamruhusu kiungo Luka Madric kuondoka. (AS)
 Mchezaji wa kimataifa wa Venezuela Salomon Rondon, 29 ambaye anachezea Newcastle kwa mkopo amewaambia Magpies kutoangalia umri wake na kumnunua kwa sababu anafanana na mvinyo.(Mirror)


 Winga wa Nice, Allan Saint-Maximin, 22, anayewaniwa na Arsenal na amefungua njia ya kujiunga na AC milan baada ya nafasi ya kujiunga na klabu hiyo mwezi januari kushindikana.


Meneja wa Blackburn Tony Mowbray amejiweka mbali na ripoti zinazozungumzwa kuhusu klabu yake kutaka kumsajili goli kipa wa zamani wa England Joe Hart, 32. Mlinzi wa Chelsea Kurt Zouma ambaye anacheza kwa mkopo katika timu y a Everton anatarajiwa kurejea Stamford Bridge kuanza maandalizi ya msimu mpya ingawa The toffees wanataka kumsajili kwa mkataba wa kudumu .


Nahodha wa Chelsea Gary Cahill, 33 na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England amemshambulia meneja wake Maurizio Sarri kwa kusema ameshindwa kumuonyesha heshima mchezaji huyo mkongwe wa Chelsea. Klabu wa Celtic imetoa ofa kwa meneja wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho, 56 kwa kumpa nafasi ya kuwa meneja wa klabu hiyo msimu ujao. (Sky Sports Italia, via Express)