Tetesi za soka Ulaya Jumatano 08.05.2019: Mbappe, Sancho, Hazard, Maguire, Asensio, Fraser


Haki miliki ya picha Getty Images Real Madrid inatarajiwa kuwasilisha ofa itakayovunja rekodi ya dunia ya £240m kwa mshambuliaji wa Paris St-Germain 20,na Ufaransa Kylian Mbappe. (France Football, via Sport)

 Mpango wa Manchester United wa kumnunua winga Jadon Sancho kwa dau la £100m umekufa baada ya timu hiyo ya ligi ya Uingereza kushindwa kufuzu katika michuano ya vilabu bingwa . (Mail)

 Hatahivyo, United watafufua hamu yao ya kumnunua beki wa Leicester na Uingereza mwenye umri wa miaka 26 Harry Maguire mwisho wa msimu huu. (ESPN)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard, 28, anafikiria kuwasilisha ombi la uhamisho ili kulazimisha uhamisho wa kuelekea Real Madrid. (AS - in Spanish)

 Chelsea tayari imekataa maombi mawili kutoka Real Madrid ili kumsajili Hazard. (Mirror) Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp kwa mara nyengine atajaribu kumsaini kiungo wa kati wa Uhispania Marco Asensio, 23, kutoka Real Madrid. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Barcelona italazimika kufanya kazi ya ziada iwapo wanataka kuingia mkataba na beki wa Ajax mwenye umri wa miaka 19 Matthijs de Ligt baada ya ajenti wa mchezaji huyo kuwasilisha mahitaji mapya ya mchezaji huyo. (ESPN)

 Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Antonio Conte amepinga kujiunga na klabu ya Roma . (La Gazzetta dello Sport - in Italian) Roma huenda badala yake ikampatia fursa mkufunzi wa sasa wa Chelsea ili kurudi nchini Itali mwisho wa msimu huu . (Telegraph)


Winga wa Uholanzi na Fulham Ryan Babel, 32, anatarajiwa kuelekea katika klabu ya Galatasaray nchini Uturuki kwa uhamisho wa bila malipo. (Sun)

 Arsenal itamwajiri aliyekuwa mchezaji wake wa zamani Edu kuwa mkurugenzi mpya wa maswala ya kiufundi katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu. (Mail)

 Kiungo wa kati wa Wales Gareth Bale, 29, pamoja na viungo wa kati wa Uhispania Marcos Llorente, 24, na Dani Ceballos, 22, wameambiwa hawatakikani katika klabu hiyo na mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane. (Marca - in Spanish)


Winga wa Uskochi Ryan Fraser, 25,anatarajiwa kusalia katika klabu ya Bournemouth msimu ujao licha ya Arsenal kutaka kumsaini. (Mirror)

 Kiungo wa kati wa Newcastle na Uingereza Isaac Hayden, 24, anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu baada ya kufeli kulazimisha uhamisho Agosti iliopita. (Telegraph)

 PSV itamuuza winga wa Uholanzi Steven Bergwijn, 21, na yule wa mexico Hirving Lozano, 23, ambao wamehusishwa na uhamisho wa Arsenal, Man United na Liverpool . (De Telegraaf - in Dutch)
 

Ombi la Manchester United la kumsajili mchezaji wa Atletico Madrid Diego Godin lilijiri mwaka mmoja mapema kulingana na beki huyo wa Uruguay , ambaye ametangaza kuondoka katika klabu hiyo ya la liga mwisho wa msimu huu . (Manchester Evening News)

 Godin, 33, amekubali kutia saini kandarasi ya miaka mitatu na timu ya Seria A Inter Milan. (ESPN) Kiungo wa kati wa Uhispania Juan Mata, 31, anataka kujiunga na Barcelona wakati kandarasi yake na Manchester United itakapokamilika mwisho wa msimu huu (Sport)