Kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer ameipa klabu yake mpaka mwakani kuuza wachezaji wote asiowataka ikiwa kama sehemu ya miango yake ya kuijenga upya klabu hiyo. (MEN)
Barcelona wameamua kuendelea na kocha Ernesto Valverde kwa msimu ujao japo kulikuwa na ripoti kuwa kocha huyo alikuwa afutwe kazi. (Marca)
Rais wa Real Madrid Florentino Perez amesema ana matumaini ya kumsajili Eden Hazard, 28, katika majira haya ya joto. (Onda Cero, via Mirror)
Newcastle United wamefanya mawasiliano na klabu ya Benfica wakiwa na nia ya kumsajili kipa wao raia wa Ugiriki Odysseas Vlachodimos, 25, na inaaminika Benfica wanataka kitita cha pauni milioni 13. (O Jogo - in Portuguese)
Kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte amesaini mkataba mpya wa kuinoa klabu ya Inter Milan mpaka mwaka 2022. (Tuttomercatoweb - in Italian)
Kocha wa Arsenal Unai Emery anataka kumsajili beki wa pembeni wa Ubelgiji Thomas Meunier, 27, kutoka katika klabu ya Paris St-Germain. (France Football)
Timu iliyopanda daraja Ligi ya Primia Aston Villa itaanza maandalizi ya michuano hiyo kwa kutuma nia ya kumsajili mshambuliaji wa Nottingham Forest Joe Lolley, mwenye thamani ya pauni milioni 10. (Mail)
Beki wa kulia wa Tottenham na England Kieran Trippier, 28, hatasainiwa tena na klabu ya Napoli baada ya timu hiyo kuelekeza nguvu zake kwa wachezaji kinda. (Sun)