Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 13.05.2019: Hazard, Coutinho, Pogba, Rice, Lacazette


Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 28, anasema kuwa amaifahamisha klabu hiyo kuhusu amuzi wake wa kuhamia Real Madrid. (Daily Mail)

Blues pia wanataka kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Philippe Coutinho, 26, ikiwa rufaa waliowasilisha kwa shirikisho la FIFA dhidi kupinga marufuku ya usajili wa wachezaji itapita msimu huu. (Cadena Ser via Daily Mail)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amefutilia mbali mkutano wa mwisho wa msimu kwasababu alikuwa amekasirika baada ya timu yake kufungwa mabao 2-0 na Cardiff siku ya Jumapili. (The Sun)


Kiungo wa kati United Paul Pogba, 26, alirushiana maneno na mashabiki baada ya wao kusema kuwa anastahili kuuzwa baada ya kushindwa na Cardiff. (Daily Mail)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 27, anasema kuwa alishangazwa na tetesi zinazodai kuwa atahamia Barcelona. (Goal)


Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini amekiri kuwa huenda akamkosa kiungo wakati wa England Declan Rice, 20, ikiwa timu kubwa zitaonesha nia ya kumnunua. (Mirror)

Meneja wa Everton Marco Silva anasema kuwa hana uhakika ikiwa klabu hiyo itashinda kinyan'ganyiro cha kumsajili kwa mkopo kiungo wa kati wa Ureno Andre Gomes, 25, msimu ujao. (Liverpool Echo)

Kocha wa klabu ya Newcastle Rafael Benitez, 59, atafanya mkutano wa dharura na mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley wiki ijayo ili kujadili hatma yake ya baadae. (Daily Mail)