VIFAHAMU VIWANJA VYA AJABU VYA MPIRA


Treni, mamba na ngome - viwanja vya ajabu vya mpira wa miguu


Hakuna viwanja viwili vya mpira wa miguu vinavyofanana.

Kutembelea kiwanja cha timu pinzani ni nafasi ya kuona mazuri, mbaya na ya kustaajabisha ambayo mchezo wa mpira unaweza kukuonesha.

Si kila uwanja duniani una mgahawa wa chakula, ama paa la kufunga na kufunguka. Klabu kadhaa zina viwanja ambavyo vina sifa za kutofautisha na kwengine.

Wiki hii nchini Uingereza, timu ambayo haishiriki ligi iitwayo ya Teversal FC's uwanja wake Tesco umejizolea umaarufu mitandaoni kwa kuwa na eneo la kuweka matoroli.

Nchini Uingereza kuna viwa nja vingi vya ajabu, lakini viwanja hivyo haviishii nchini humo tu.

Je unajua kuna uwanja ambao ndani yake inapita treni, kando tu ya eneo la kuchezea na kabla ya jukwaa la mashabiki.

Huo ni uwanja wa klabu ya TJ Tatran Cierny Balog, inayocheza mpira wa ridhaa nchini Slovakia.

Mashabiki katika uwanja huo mara kwa mara wanakatishwa uhond wa kutazama mechi kwa garimoshi linalokatiza likiendelea na safari zake.Na nchini Qatar kuna timu inaitwa Al-Shamal SC. Japo kuna timu nyingi zinabatiza viwanja vyao majina ya ngome, kwa klabu hiyo ya Qatar, huo ni uhalisia. Kiwanja chao ni ngome.


Hata hivyo, hata ngome si ajabu kuwa kiwanja kama ilivyo kwa umbo la mnyama.

Mwaka 2015, klabu ya Bursaspor ilizindua uwanja wake ufahamikao kwa jina rasmi kama Uga wa Buyuksehir Belediye ama maaarufu zaidi kwa jina la utani 'Timsah Arena' ikimaanisha 'Uga wa Mamba'

Ni kiwanja kizuri, na kimetengenezwa kwa bajeti ya chini pia.Je, viwanja hivyo vinalingana vipi na viwanja vya ajabu barani Afrika. Ama ndiyo ikstaajabu ya Musa utayaona ya Firauni.