Je ni nini kilichotokea?
Haki miliki ya pichaREUTERS Ruiz ambaye alishirikishwa katika pigano hilo baada ya raia wa Marekani Jarell Miller kupatikana na dawa za kusisimua misuli wiki sita tu kabla ya pigano hilo. Na ilipofikia raundi ya saba , wakati Joshua alipoangushwa mechi hiyo ilikuwa imekwisha baada ya kupigwa ngumi nyingi zilizomchanganya na kulazimika kutema kifaa kinacholinda meno. Hakuwa nacho mdomoni na refa alipoona Joshua kachanganyikiwa aliingilia kati na kusitisha pigano. Ruiz alionekana hafifu sana kuweza kumshinda bingwa huyo wa ndondi sio tu kwa maneno bali hata kwa maungo. Waingereza watakapoamka siku ya Jumapili alfajiri watashangazwa na matokeo haya. Pigano la marudio kabla ya mwisho wa mwaka Joshua alikuwa ameshindwa katika raundi pili akishinda moja wakati alipopigwa knockout lakini atapata fursa ya kujirekebisha katika mechi ya marudio jijini London , kabla ya mwezi Disemba kulingana na promota Eddie Hearn.
Hakimiliki ya Picha @anthonyfjoshua@ANTHONYFJOSHUA Hakimiliki ya Picha @MoSaleh8@MOSALEH8 Hakimiliki ya Picha @StephenMcIner82@STEPHENMCINER82 Kwa sasa mazungumzo yoyote ya kuzipiga dhidi ya Tyson Furry ama hata Deontay Wilder yamesitishwa. Ruiz ambaye kwa sasa ameshinda mara 33 na kupoteza mara moja aliruka ruka katika ukumbi wa ndondi wa Madison Square Graden baada ya refa kusitisha pigano hilo. Anajiunga na James Buster Douglas ambaye alimshangaza Tyson na Hasim Rahman ambaye alimpiga Lewis mwaka 2001 kama mmojawapo wa mabondia walioushangaza ulimwengu. Lewis alijibu kwa kushinda pigano la marudio. Ruiz hatahivyo alionyesha uwezo mkubwa katika pigano hilo ikimaanisha kwamba Joshua atakuwa na kazi ya ziada kumshinda katika pigano hilo linalotarajiwa kufanyika kabla ya mwaka kukamilika mjini London