Manchester United wamekubali kulipa ada ya pauni milioni 55 kumsajili mlinzi wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka, 21. (Record)
Hata hivyo madai hayo yamekanushwa huku vilavu hivyo vikiendelea kushauriana kuhusu usajili wa kiungo huyo. (Mail)
Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar amekuwa akitafuta nyumba mjini Barcelona,licha ya tetesi kuibuka kuwa nyota huyo wa Kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 anajiandaa kurejea Nou Camp. (Sport)
Kiungo wa kati wa Brazil Jorginho yuko tayari kuondoka Chelsea na kwenda kujiunga na Maurizio Sarri katika klabu ya Juventus mwaka mmoja baada ya kusajiliwa na Napoli kwa kama cha pauni milioni 50. (Mirror)
Inter Milan na Atletico Madrid wanataka kusajili beki wa England anaechezea klabu ya Southampton Ryan Bertrand, 29. (Mail)
Juventus wanaamini wataipiku Real Madrid katika usajili wa kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Mirror)
Sporting Lisbon wanashauriana na Liverpool kuhusu usajili wa winga wa Ureno wa miaka 19, Rafael Camacho. (Standard)
Norwich wanamatumaini ya kumnunua beki wa England Max Aarons, 19, licha ya mchezaji huyo kunyatiwa na Manchester United. (Telegraph)
West Ham wameifahamisha Manchester United na Manchester City kuwa hawana mpango wa kumuuza nyota wa Kimataifa wa England anaecheza safu ya kati Declan Rice, 20, msimu huu wa joto. (Sky Sports)
Kipa Tom Heaton amekataa ofa ya kandarasi mpya aliyopewa na Burnley. Kipa huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 33 ataingia mwaka wake wa mwisho wa mkataba wake wa sasa katika uwanja waTurf Moor mwezi ujao. (Guardian)