ALI KIBA AMPA TALAKA TATU MKE WAKE


Msanii Alikiba a.k.a King Kiba amempa talaka tatu mkewe Amina Khalifa raia wa kenya baada ya kushindwa kupata muafaka juu ya ugomvi wao na ndugu wa Alikiba na Mama wa Alikiba.
 Ndoa ya King Kiba ilianza kuingia dosari baada ya Amina kutaka ndugu wa Alikiba wakajitafutie maisha yao na wajitegemee jambo ambalo lilizua taharuki na ugomvi mkubwa baini ya ndugu wa Alikiba na Amina..
 Amina alidai ni vigumu kuishi na watu wengi vile ndani ya nyumba moja ambapo mpaka wasanii wake wa Kings Music Wanaishi Humo humo, hata kama ni ghorofa na bado kuwe na amani...hivyo alimshauri alikiba awape mitaji wakajitegemee au awapangie nyumba nyingine.....
 Hili jambo liliendeleza mgogoro mkubwa hadi Mama Alikiba kuingilia kati na kutaka Alikiba amuache Amina na akadai hapendi hata watoto wa Alikiba wakubwa kuwa pale..