RAIS MAGUFULI ATUMBU MKUU WA WILAYA NA MKURUGENZI WAKE..


Leo September 17, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro Majura Mateko Kasika na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mussa Elias Mnyeti. Uteuzi wa viongozi hao umetenguliwa kuanzia leo September 17, 2019. Uteuzi wa viongozi watakaojaza nafasi hizo utafanyika baadaye.