Tetesi za soka Ulaya Jumapili 15.09.2019: Messi, Kroos, Pogba, De Gea, Eriksen, Mane


Mchezaji nyota wa zamani wa England, David Beckham ameongezea nguvu mipango yake ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi.


Ningependa kumuona Neymar akirejea - Messi Beckham anamiliki klabu ya soka nchini Marekani ijulikanayo kama Inter Miami, ambayo imeshatuma wawakilishi wake kuzungumza na baba wa Messi. (Sun on Sunday)

 Inter Miami pia wanataka kumsajili winga wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales, Gareth Bale, 30.(Maxifoot - in French)


Manchester United wanapanga kumsajili kiungo Mjerumani wa klabu ya Real Madrid Toni Kroos, 29, mwezi Januari katika mkataba wa kubadilishana wachezaji.
 United wanaweza wakamtoa Paul Pogba na kukubali kiasi cha pesa kama sehemu ya makubaliano hayo. (Bild - in German) Kipa wa Uhispania David de Gea, 28, ametia saini mkataba mpya wa miaka minne na Man United wa thamani ya pauni 250,000 kwa wiki, na malipo yanaweza kupanda mpaka pauni 350,000 kwa wiki kulingana na kiwango cha mchezo. (Sunday Mirror) 

Mshambuliaji wa England Callum Hudson-Odoi, 18, anatarajiwa kuingia makubaliano mapya na klabu yake ya Chelsea mara baada ya kupona majeraha yake. (Sun on Sunday)

 Liverpool wameanza mazungumzo ya kuongeza mkataba na mshambuliaji wake raia wa Senegali Sadio Mane. (SoccerLink, via Sport Witness)


Kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 27, anasubiria uwezekano wa kuihama klabu ya Tottenham na kuelekea Real Madrid, mwezi Januari. (Marca - in Spanish)

 AC Milan na Inter Milan wote wana mipango ya kumsajili kiungo Mserbia Nemanja Matic, 31, kutoka Manchester United mwezi Januari. (Corriere Dello Sport - in Italian)
 
 Manchester United wametuma wachunguzi wake kumuangalia mshambuliaji wa Fenerbahce ya Uturuki Vedat Muriqi, 25, wakati akiichezea timu yake ya taifa ya Kosovo dhidi ya England wiki iliyopita. (Sunday Express)


Kocha wa Newcastle Steve Bruce amepewa ridhaa na uongozi wa klabu ya kusajili wachezaji wapya mwezi January, hususani mawinga. (Chronicle)
 Mshambuliaji wa Juventus na Croatia Mario Mandzukic, 33, ambaye alikuwa akihusishwa na kutaka kuhamia Man United hivi karibuni, anakaribia kukamilisha usajili wa kuelekea Marekani katika klabu ya LAFC. (Calciomercato)
 Beki raia wa England Tyrone Mings, 26,amesema alishangazwa sana pale Aston Villa walipoamua kumsajili kwa pauni milioni 20 kutoka klabu ya Bournemouth. (Express and Star)