TETESI ZA USAJILI: MADDISON, WILLIAN, COUTINHO, LOVREN, CEBALLOS
 Manchester United, inaweza kuelekeza nguvu kumsajili kiungo wa Leicester City na England, James Maddison, 23, baada ya kumuwinda kwa muda mrefu nahodha wa Aston Villa, Jack Grealish, 24, ambaye ameonesha utovu wa nidhamu nje ya uwanja, kwa kushindwa kufuata maagizo ya serikali ya kukaa nyumbani katika kipindi hiki cha mlipuliko wa virusi vya Corona. ((Daily Star).

 Liverpool, haina nia ya kumsajili tena kiungo wa Brazil, Philippe Coutinho, 27, anayecheza kwa mkopo Bayern Munich kutokea Barcelona. (Mirror).

 Real Madrid, inamuwinda “Kaka mpya’ wa Sao Paulo, Igor Gomes, 21, huku Barcelona, Sevilla na Ajax, nazo zikimtupia jicho kiungo huyo anayecheza timu ya taifa ya Brazil chini ya miaka 20. (AS). Kiungo wa Chelsea na Brazil, Willian, 31, ataendelea kucheza ligi kuu England, hata kama ataondoka Stamford Bridge na huenda Arsenal na Tottenham zikaanza mipango ya kumnasa. (ESPN Brazil).

 Arsenal, Tottenham na West Ham, zimeonesha nia ya kumsajili mlinzi wa Liverpool, Dejan Lovren, 30, ambaye anaonekana kuwa na nafasi ndogo ya kubaki Anfield. (Teamtalk).

 Mlinzi anayecheza kwa mkopo Arsenal, Dani Ceballos, 23, anaweza kurudi Real Betis kuliko kuendelea kubakia Emirates, na hii ni endapo timu yake ya Real Madrid, haitataka kumrejesha Santiago Bernabeu. (Estadio Deportivo kupitia Express).

Post a Comment

0 Comments