Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 15.04.2020


Inter Milan inamtaka kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 29, kwa kumbadilishana na mshambuliaji Lautaro Martinez ikiwa Barcelona itamnyakua kiungo huyo wa Argentina wa miaka 22 kutoka kwao. (La Gazzetta dello Sport, via Marca)

 Barcelona itajaribu kumsajili mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 20, kutoka Real Sociedad wakimkosa Martinez. (Marca)

Kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, 29, ni miongoni mwa wachezaji watatu wanaolengwa na Real Madrid. (AS, via Mail)


N'Golo Kante, 29, ni miongoni mwa wachezaji watatu wanaolengwa na Real Madrid Mkufunzi wa zamani wa Tottenham Harry Redknapp anasema mshambuliaji wa Spurs Harry Kane hatahamia Manchester United lakini nahodha huyo wa England "huenda akapendelea" kujiunga na Barcelona ama Real Madrid "siku moja". (Talksport)

 Arsenal na Chelsea watapewa nafasi ya kumsajili kiungo wa kimataifa wa Barcelona Philippe Coutinho msimu huu wa joto, huku Bayern Munich wakijiandaa kubadili mkataba wake wa mkopo kuwa uhamisho wa kudumu. (Sun)


Arsenal na Chelsea kupewa nafasi ya kumsajili kiungo wa kimataifa wa Barcelona Philippe Coutinho Manchester United inamfuatilia kiungo wa kati wa Atletico Madrid Saul Niguez lakini iko tayari kulipa £70m kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa paundi milioni 132. United wanatarajiwa kuongeza marupurupu yake kwa kati ya £115,000-a- hadi karibu £200,000 kwa wiki. (Sun)

 Wakala wa kiungo wa kati wa Ajax midfielder Donny van de Beek, andasema mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi wa miaka 22- amabye anahusishwa na tetesi ya kuhamia Real Madrid na Manchester United,ananyatiwa na "klabu kadhaa. (Voetbal International, via Metro)


Sergio Aguero anatakiwa na klabu yake ya zamani ya Independiente Klabu ya zamani ya mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, Independiente imeongeza juhudi ya kutaka kumrejesha tena nyota huyo Argentina wa miaka 31 katika klabu hiyo. (Mirror)

 Mashambuliaji wa Italia Lorenzo Insigne, 28, anajiandaa kurefusha mkataba wake na Napoli hadi 2025. (Calciomercato)