Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 16.01.2021: Rice, Tomori, Drinkwater, Garcia, Lacazette

Manchester United wanajiandaa kumenyana na Chelsea katika mbio za kumsaka kiungo wa kati wa West Ham Muingereza Declan Rice, 22, msimu ujao. (ESPN)

 AC Milan wanataka kupewa nafasi ya kumnunua mchezaji wa Chelsea na England wa safu ya kati na nyuma Fikayo Tomori ikiwa watamsajili kwa mkopo mwezi huu. Klabu hiyo ya Italia huenda wakaliba karibu £26m kumpata nyota huyo aliye na umri wa miaka 23. (Guardian) 

Kiungo wa kati wa Chelsea Muingereza Danny Drinkwater, 30, anakaribia kutia saini mkataba wa mkopo kujiunga ba klbu ya Kasimpasa ya Uturuki baada ya nyota yake kufifia tangu alipotia Stamford Bridge kwa uhamisho wa kima cha £35m kutoka Leicester mwaka 2017. (Mail)
Mchezaji wa Chelsea Danny Drinkwater wakati alipokuwa Leicester Pep Guardiola anasema Mhispania Eric Garcia anayecheza safu ya kati na nyuma huenda akaondoka Manchester City katika uhamisho wa Januari. Mkataba wa kiungo huyo aliye na umri wa miaka 20 unakamilika mwisho wa msimu huu na ananyatiwa na klabu yake ya zamani Barcelona. (Sky Sports) 

 Wagombea watatu wa urais wa Barcelona wamekubaliana kuahirishwa kwa uchaguzi kutoka Januari 24 hadi Machi 7 baada ya mashariti mapya ya kukabiliana na Covid-19 kubuniwa katika eneo hilo. (AS)
Eric Garcia wa Man City huenda akarejea klabu yake ya zamani Hatua hiyo inamaanisha Barcelona huenda ikasubiri hadi mkataba wa Garcia utakapokamilika msimu wa jota kumsajili ajiunge na klabu hiyo, kwani klabu hiyo haina uwezo wa kumwachia aondoke kwa uhamisho wa bure Januari hii. (Marca) 

Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone anatafakari uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, baada ya uhusiano wa nyota huyo aliye na umri wa miaka 29 na meneja wake Mikel Arteta kuyumba. (AS - in Spanish)
Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette Everton wanataka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Bayern Munich Joshua Zirkzee,19, na huenda baadae wakamnunua. (Mail) 

Bournemouth wako tayari kumpatia mkataba kiungo wakati wa zamani wa Arsenal na West Ham Jack Wilshere, 29. Mchezaji huyo wa kimataifa wa England amekuwa akifanya mazoezi na Cherries kwa muda wa wiki tatu zilizopita. (Talksport)
Bournemouth kumsajili kiungo wakati wa zamani wa Arsenal na West Ham Jack Wilshere Marseille wanajadiliana na Napoli kumhusu mshambuliaji wa Poland Arkadiusz Milik, 26, ambaye pia ananyatiwa na Juventus na Atletico Madrid. (Goal)

Post a Comment

0 Comments