GERALD PIQUE, BARCELONA NI MUHIMU KULIKO MIMIGERALD PIQUE, BARCELONA NI MUHIMU KULIKO MIMI
.
Dakika chache tu Barcelona wametoka kupokea kipigo cha mabao nane kutoka kwa Bayern Munich, alihitajika mtu wa kuzungumza na waandishi wa habari. 

Wakiwa vyumbani wamepoa hakuna anayemsemesha mwenzake, kila mmoja anafikiria kilichotokea, Gerald Pique alikubali kubeba msalaba ambao hadi captain Lionel Messi aliukataa.

Akaelekea kwenye chumba cha mahojiano. Thomas Muller akiwa pembeni yake alisema, "Sisi tunasahau huu ushindi na kuifikiria nusu fainali. Mabao nane robo fainali ni ujinga kama hatutabeba kombe." 

Hayo yalikuwa maneno ya mwanaume wa kijerumani, anayejua misingi ya soka la kijerumani. Hakuna aliyekuwa na hamu na sauti ya Muller sana, wote walitaka kusikia kutoka kwa muhanga wa kipigo, ana nini cha kusema??

Gerrald Pique, macho yakiwa makavu alifungua mdomo wake kuzungumza akasema, "Fedhea! Ndilo neno zuri la kutumia. Aibu! Ndilo neno la kutumia hapa."

"Nadhani tunahitaji mabadiliko makubwa, si kwa wachezaji tu bali kila mahali. Sitaki kutaja watu kwa majina, lakini tunahitaji mabadiliko makubwa"

"Kama ni damu ngeni inahitajika ili kubadili huu upepo, basi nitakuwa wa kwanza kufungasha virago vyangu na kuondoka ili tu Barcelona irudi katika hali yake". Alimaliza Pique.

Hii sentensi ya mwisho ilibeba vichwa vya habari vya magazeti asubuhi iliyofuata. Hii sentensi ya mwisho ilibeba hisia za WaCatalonia na kuwapa picha nini kinahitaji kufanyika.

Gerald Pique aliukubali ukweli mchungu ambao si rahisi kwa binadamu wa kawaida kuukubali. Tofauti na kuwa mchezaji wa Barca, yeye ni shabiki mkubwa wa Barcelona. Barcelona ni nyumbani kwake lakini yupo tayari kuondoka ili klabu yake pendwa isonge mbele. Only Legends can do that💪.

Gerald Pique is 34 today. Happy birthday Gerald Pique. 
.
✍ #salushinetz

Post a Comment

0 Comments