Graham Potter Master class
Graham Potter Master class 

Unaweza kuchagua hata wachezaji 6 mpaka 7 kuwapa Man of the Match kutoka kikosi cha Brighton leo 

✍Kocha Potter kapatia kwa 100% mbinu zake leo , kafunga njia zote za katikati ya uwanja  na kuwaachia Liverpool kupiga krosi akijua kabisa Webster , Dunk na White watapambana na mipira yote ndani ya boksi 

✍Kwenye kiungo hasa Boussuma hakupaniki wala kuwa na wasiwasi pale alipokuwa akipokea mipira kutoka kwa mabeki wake , alihakikisha inafika kwa Gross na Trossard ...ambao ndio walikuwa " Ball Carriers " wanachukua mipira na kukokota kwa haraka mpaka kwa Maupay.

✍Liverpool mara nyingi walikuwa taratibu sana kwenye kusuka mashambulizi , na hata ikifika mbele Shaqiri anageuka anapiga tena ' back pass ' , Firmino anachelewa kupiga shuti golini , Salah alinyimwa kabisa ' Space ' ya kukokota mpira au kupiga golini ...unaweza ukajiuliza mara ngapi kipa wa Brighton alifanya saves zaidi ya mbili za hatari ?? 

✍Na kiukweli Brighton walitengeneza nafasi nyingi za kufunga nzuri zaidi ya Liverpool. Wamestahili pointi zote tatu

NOTE : 

Timu zenye majina yanayoanzia na herufi " B " yanachukiwa sana pale Anfield ( Burnley na Brighton )

Post a Comment

0 Comments