HOFU INAKUCHELEWESHA KUISHI KWENYE KUSUDI LAKO.

HOFU INAKUCHELEWESHA KUISHI KWENYE KUSUDI LAKO. 
Umeshawahi kujiuliza kwanini chizi haumwi anapokula vitu vichafu lakini mwenye akili huwa anaumwa anapikula vitu vichafu?. Je unadhani ni kipi kinachomfanya mgonjwa wa akili asiumwe wakati yeye anamwili kama wako na ana tumbo kama lako?.

Kitaalamu mtu anapokuwa ana tatizo la akili yaani hana akili vizuri kuna baadhi ya hofu huwa zinaondoka kwenye akili yake. Huwa hafikirii matokeo ya alichofanya ila huwa anafanya anachoona sawa kufanya kwa wakati huo anaofanya. Chizi au mgonjwa wa akili huwa haumwi kwasababu hana hofu ndani ya moyo wake ndio maana hapati madhara kama anayopata mtu timamu anapofanya kitu cha madhara. 

Hofu ndio adui mkubwa na anaweza kukutengenezea maradhi hata sehemu ambayo haina maradhi. Licha ya kuwa dunia inapitia kwenye changamoto ya maradhi hatari ya corona lakini hofu pia inachangia idadi ya vifo kuongezeka. Sikwambii usichukue tahadhari hapana chukuwa tahadhari ila ondoa hofu.

Hofu ndio inayokufanya ushindwe kufanikiwa miaka yote kwasababu unaamini kuwa chochote utakachokifanya hakiwezi kuwa. Hofu inakufanya kila siku kuzalisha migogoro kwenye ndoa yako kwasababu umempenda mtu ambae humuamini hivyo unahofu nae. 

Siku utakayoondoa hofu akilini mwako utastaajabu namna milango ya fursa itakavyofunguka. Jifunze kutoka kwenye matatizo ya wengine lakini usihofu kutenda eti kwasababu wengine walianguka walipotenda. Hofu inaweza kumuua mgonjwa kitandani hata kama vipimo vinaonesha hana tatizo. Ondoa hofu ili ufanikiwe kwasababu wenye hofu huwa hawafanikiwi.

#salushinetz

Post a Comment

0 Comments