Kama wanapiga vile kumbe wanafinya ....City hao

Kama wanapiga vile kumbe wanafinya ....City hao 

Hili jeshi la Pep Guardiola halina masihara , linafumua tu kila atakayekatiza kwenye 18 zao, halafu inachotia hasira ni kwamba hawashindi kwa magoli mengi sanaaaaa, uimara wao upo zaidi kwenye safu yao ya ulinzi . Ni clean sheet baada ya Clean Sheet . Mpaka maji tuite Mma .!!! 😂😂

✍🏼Hivi Bernardo Silva ana mapafu mangapi ?? Yupo kila sehemu , anacheza kwa intensity ya hali ya juu sana, anakimbia sana, ana press sana na bado anakuwa na ubora wa kupiga pasi na kulinda mpira .

✍🏼Ilkay Gundogan ameweka ndimu. Kila mechi sasa kama hajafunga basi katoa pasi ya goli . Hakuna Kevin De Bruyne kaamua kuchukua majukumu yeye . GOOD GAME .

✍🏼Gabriel Jesus, Raheem Sterling, Cancelo , Stones , Dias wachezaji wengi walicheza vizuri sana leo . Pole kwa Burnley 

✍🏼Burnley wamekuwa na bahati mbaya ya kukutana na timu mbili bora zilizowazidi sana ubora katika mechi mbili mfululizo ( Chelsea na City ) sasa waangalie sehemu gani nyingine ya kuokota pointi. 

NOTE : 

1: Kwani hawa Burnley waliwafungaje wale jamaa ?? 🤔🤔

2: Wikiendi itakuwa tamu sana ( Mabingwa watetezi Vs Vinara wa ligi )

#salushinetz

Post a Comment

0 Comments