KILA MWANAMKE ANAHOFU YA ULINZI NDANI YAKE.

KILA MWANAMKE ANAHOFU YA ULINZI NDANI YAKE. 

Kila mwanamke ana (Fear of protection) hii ni ile hofu ya ulinzi ambayo ipo ndani yake. Moyo wa mwanamke huwa ni rahisi sana kugundua mabadiliko ya mwanaume kitabia hasa anapokuwa kahamisha upendo moyoni mwake na kupenda sehemu nyengine. 

Mara zote ndio maana hupenda kumuuliza mumewe (Baby do you love me?.) Hii haimanishi kuwa hakuamini kama unampenda hapana, bali hupenda uhakika  wa salama ya pendo lake kwa kukuuliza  mara kwa mara. Moyo wa mwanamke ukipenda unaumia na ukiachwa unaumia zaidi ndio maana takwimu za kidunia zinaonesha wanawake wengi wanajiua kwasababu ya mapenzi.

Mwanamke akipenda huwa anatoa  bustani ya adeni ya penzi lake kumkabidhi mwanaume aliompenda ndio maana akisalitiwa huwa ni mvivu sana kusahau maumivu ya usaliti. Huwa anafikiri na kusema kwa sauti ya moyo wake  hivi kwanini kanisaliti na kuniacha wakati mimi nilimpenda kwa dhati?.

Hii ndio hupelekea kujiona labda anakasoro fulani ambazo hata akiolewa na mwengine yatakuwa yaleyale tu. Anachukia ndoa na kuwachukia wanaume hata kama atajitokeza mwema kwake yeye hutafsiri wanaume wote ni sawa.

Tuipe nafasi na kuitunza mioyo ya wanawake kwasababu hawana sehemu nyengine pakutuliza na kuziaminisha nafsi  zao zaidia ya kwetu wanaume. Mungu alituumba watu wa aina mbili tu mwanaume na mwanamke. Sasa kumuumiza mwanamke ili upate manufaa ya mwili ni eneo la dhambi na uzalilishaji kwa jinsia ya kike. 

#salushinetz 

Post a Comment

0 Comments