MAKEUP HAWEZI KUZIDI IBADA KWA KUPENDEZESHA.

MAKEUP HAWEZI KUZIDI IBADA KWA KUPENDEZESHA. 

Mwanamke ambae anatawadha kila siku mara tano kwa ajili ya swala hana haja ya Mekup kung'risha uso wake.  Mng'aro  anauweka Mola kwenye uso wa mwanamke mfanya ibada huwa haufutiki hata uso wake ukiloa na maji.  Dunia imekuwa na nguvu kiasi cha wanawake wengi kusahau jambo la ibada.

Unaweza sema wao waliumbwa kuja kujipamba na kutupia Instagram pamoja na kuchambana. Kumbe jambo la kuabudu ni jambo la kila kiumbe anapaswa kufanya ibada kwa ajili ya kesho yake. Tafiti nyingi za kisayansi zimeonesha kuwa watu wenye kumtegemea Mungu mara kwa mara huwa na furaha nyingi na hawapo hatarini kupata depression.

Mara zote huwa nasema jamii ipo chini ya nyayo za mwanamke akitengemaa mwanamke na kuwa bora basi changamoto nyingi sana kwenye jamii zitapungua. Lakini kama mwanamke hatojua ni kipi kiatu chake akavaa kila kiatu basi ni ngumu kupata jamii yenye natija. 

Kama unaamini kuna maisha baada ya haya huwezi kuchukia wala kupuuza ibada hata kidogo. Hitajio la mwili ni chakula ambacho ndio tunakipigania usiku na mchana lakini hitajio la moyo ni imani ikiambatana na ibada. Maisha bila Mungu ni sawa na mdomo bila meno sehemu ya kutafuna  utamung'unya.

Lazima muda wote uwe na hofu ya Mungu kukaa uchi mitandaoni hakuwezi kukusaidia chochote kwenye maisha yako zaidi ya kuonekana limbukeni na hukustaharabishwa kwenye malezi yako. Kuwa mama bora ni mchakato unaosukwa toka ukiwa msichana jitahidi kuijua hadhi yako ili idumu heshma yako. 

#salushinetz

Post a Comment

0 Comments