PHIL FODEN, PEP GUARDIOLA HAJAWAHI KUELEWEKA

PHIL FODEN, PEP GUARDIOLA HAJAWAHI KUELEWEKA
.
Mbele ya waandishi wa habari na kingereza chake cha kuokota Pep Guardiola akasema, "Phil Foden is the greatest talent I have ever managed". Hakuna aliyemuelewa Pep Guardiola, hata mimi sikumuelewa.
.
Subiri kwanza, huyu ndiyo mtu aliyempandisha Messi kutoka La Masia pale Barcelona, huyu mtu amemfundisha Andres Iniesta, huyu mtu anafanya kazi na David Silva na Kelvin De Bruyne. Anamaanisha kweli kuhusu Foden??
.
Labda kingereza kinampiga chenga, labda lugha ya malkia inamkataa, labda alitaka kuzungumza vingine lakini tulimuelewa tofauti kwasababu hii si lugha yake ya kwanza.
.
Lakini hapana Pep Guardiola hakuwa na masihara, alikuwa anamaanisha. Siku David Silva anatangaza kuondoka Pep Alirejea tena kusema, msiniulize namsajili nani kuziba nafasi ya Silva, pengo la Silva tumeshaliziba, yupo Phil Foden, ana kipaji kuliko David Silva.
.
Hakuna aliyemuelewa tena, tulijua tu ni Pep na zile stori zake za kumkataa Toni Kroos kwasababu anapenda sana kufunga kutokea mbali badala ya kupiga pasi za mwisho kwa washambuliaji. Hakuna aliyewahi kumuelewa Pep. Muulize hata Thierry Henry na bao lake la kwanza Barcelona (Kesho nitakuletea hiki kisa).
.
Siku zinaenda na muda haugandi, Foden kwenye kiungo cha Manchester City anasahaulisha kuwa David Silva ameondoka The Citizens na Kelvin de Bruyne yupo juu ya kitanda cha hospitali anapatiwa matibabu.
.
Phil Foden ana miaka 20, Pep alimzungumzia akiwa na miaka 17. Pep alitudanganya au kutuambia ukweli?? Tunaogopa kujibu kwasababu hakuna aliyewahi kumuelewa Pep.
.
Pichani kushoto ni mtoto Phil Foden akiokota mipira Etihad mechi dhidi ya Liverpool. Pichani Kulia ni Phil Foden akiwafunga Liverpool Anfield. Man City wanashinda kwa mara ya kwanza Anfield tangu 2003. Foden akiwa na miaka mitatu tu.
.

Post a Comment

0 Comments