RONALDO DE LIMA, MUAMALA HAUKUTHIBITISHWA 1994

RONALDO DE LIMA, MUAMALA HAUKUTHIBITISHWA 1994
Kila mtu pale Granja Comary alivutiwa sana na uwezo wake mpaka wachezaji walihusudu sana ubora wa kijana huyo Mdogo, lakini tukumbuke ulikuwa ni mpango wa siri wa Viongozi kuwa aende tu kupata uzoefu atumike michuano mingine ijayo

Taarifa zilivuja baadhi ya maeneo mfano Boa Vista ni sehemu ambayo Mashabiki wake hutazama mpira ufukweni, wanahusudu sana mpira burudani ni moja kati ya eneo la chimbuko la Samba kwenye mpira wao, hawa walianza kupiga kelele

Hatimae siku ikafika Kikosi cha Brazil kinaelekea Marekani kwa ajili ya kombe la dunia 1994, Ronaldo de Lima  na begi lake huku washikaji zake kutoka mtaani pale Rio de Janeiro wakimsindikiza kwa macho wakiwa na matumaini makubwa sana

Timu ilipowasili Marekani kumbuka kulikuwa na bifu kubwa sana kati ya Romario na Bebeto, siku moja Romario alimuita DE LIMA baada ya watu wote kumaliza mazoezi, akaanza kumwambia "wewe ni Mwanasoka ila ukitaka kuwa Mwanasoka bora iga nachofanya uwanjani"

Siku inayofuata tena baada ya mazoezi, aliitwa na Bebeto mwenye bifu kubwa na Romario, akamuuliza De Lima "Unafahamu nini kuhusu timu ya Taifa ya Brazil?" De Lima akamjibu kitoto tu kuwa ni timu kubwa na ndoto ya kila mtu,  Bebeto akamalizia "Mwenye ndoto ya kusahau yote kwa ajili ya Taifa hili"

Ndipo baadae sana RONALDO akaja kugundua hawa wawili wana bifu kubwa sana ila bado uwanjani Bebeto atapangua ukuta atapiga pass kwa Romario, atafunga na watashangilia pamoja, bado Bebeto anaweza kuonewa ila Romario angeenda kumtetea licha ya ugomvi wao

Brazil walifanya makubwa sana michuano ile na wakafika hatua ya fainali dhidi ya Italia ya Field Marshal Franco Baressi, fainali ilikuwa ngumu sana Romario na Bebeto walifanya kila kitu ila walifeli kwakuwa Waitaliano waliwafahamu vyema sana, ila ghafla wakamuona mtoto mdogo anapasha

Kila Mchezaji wa Italia alishangaa sana ni nani yule Mtoto? Ana ubora gani mpaka kuitwa Brazil? Wakaanza kutetemeka ila hakupata nafasi ya kuingia na mechi ikaisha kwa ushindi wa matuta kwa Brazil, Kwanini walimnyanyua Ronaldo apashe? Walikuwa na maana ni Mwisho wa zama ya wakina Romario sasa anafuata RONALDO DE LIMA

#salushinetz

Post a Comment

0 Comments