RONALDO; NJE YA UWANJA, NJE YA PESA NA UMAARUFU ANAISHI BINADAMU MWEMA.
RONALDO; NJE YA UWANJA, NJE YA PESA NA UMAARUFU ANAISHI BINADAMU MWEMA.
.
Ukumbini alikuwepo Jose Mourinho na mpinzani wake wa karibu wa miaka mingi, Josep 'Pep' Guardiola. Mourinho alichangia dola elfu 35 za kimarekani, Pep Guardiola na yeye alitoa elfu 35 dola. Wote wawili kwa pamoja walitoa jumala ya dola elfu 70.
.
Ilikuwa London 2017, katika ghafla iliyoandaliwa na taasisi ya 'Make a wish'. Lengo lao kubwa ni kuwasaidia watoto wanaougua magonjwa hatari. Lengo lao kubwa ni kuwapa nafasi ya pili ya kuishi watoto walio hatarini kupotea kwa magonjwa hatari. Kumbuka naizungumzia taasisi ya msaada ya 'make a wish'.
.
Walikuwepo matajiri wengi, walikuwepo watu maarufu wengi, wanamuziki, viongozi wa dini, wachezaji na watu wengine wenye ushawishi mkubwa duniani. Lengo ni kuchangisha pesa kwa ajili ya kusaidia watoto wasio na tumaini la kuishi kwasababu ya magonjwa sugu.
.
Baada ya Mourinho na Guardiola kuchangia dola 35,000 kila mmoja. Walizungukiwa watu wengine, kila mmoja alitoa kadiri alivojipanga kutoa. Walioshindwa kufika walituma wawakilishi.
.
Ilifika saa ya kujua Ronaldo ametoa kiasi gani, kila mtu alitega sikio kusikia staa wa dunia anatoa kiasi gani. Kumbuka ukumbini walikuwepo matajiri wakubwa mara 10 zaidi yake. Walijua hatawazidi kiasi anachotoa lakini walitamani tu kusikia kwasababu ya jina lake.
.
Kwa mshangao mkubwa Ronaldo hakutoa pesa, unajua kwanini?? Pesa haikuwa kitu cha thamani zaidi kwake. Alitoa replica ya tuzo ya ballon d'or aliyoshinda 2013. Akasema ifanyiwe mnada kisha pesa inayopatikana ndiyo mchango wake.
.
Ballon d'or yake ya 2013 ilinunuliwa na tajiri namba moja wa Israel, Idan Ofer. Iliuzwa zaidi ya dola laki saba za kimarekani. Pesa ikaenda kuwasaidia watoto wanaoteseka na cancer huko Indonesia.
.
Kwa Ronaldo, ballon d'or ndiyo tuzo ya thamani zaidi kwa mchezaji yoyote lakini haina thamani kama maisha ya binadamu wengine. Aliona hakuna sababu ya kufurahia kuiona ikiwa kabatini kwake, wakati wapo watu wanahitaji zaidi.
.
Akaamua kuitoa ili kuihamasisha dunia ichangie pesa kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye uhitaji.
.
Binadamu mwema Cristiano Ronaldo ana miaka 36 leo🙏.
.
✍ #salushinetz

Post a Comment

0 Comments